Brimin Kipruto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Brimin Kipruto:mwanariadha maarufu wa mbio ya 3000m wa Kenya Kenya

Brimin Kipruto (alizaliwa Korkitony, Wilaya ya Keiyo, 31 Julai 1985) ni mwanariadha wa umbali wa wastani wa Kenya.

Alishiriki hasa katika mbio ya 3000m ya kuruka viunzi ambapo muda wake bora kabisa ni dakika 8:04.22.

Katika Mbio za Dunia za Vijana za 2001 mjini Debrecen,Hungaria alikuwa nambari ya pili katika mbio ya 3000m ya kuruka viunzi. Yeye alimaliza masomo yake ya shule ya upili hapo 2003 kutoka Shule ya Sekondari ya Kipsoen. Mwaka uo huo alishiriki katika Mbio ya Vijana ya Afrika nchini Kamerun na akashinda medali ya fedha.Hapo mwaka wa 2004,katika Mbio ya Vijana ya Afrika alishiriki katika mbio ya 1500m badala ya yake ya kawaida na akawa #3.

Brimin Kipruto akibeba bendera ya Kenya baada ya mbio

Ilpofika mwaka wa 2004, baada ya kumaliza # 2 katika majaribio ya Olimpiki ya Kenya,Kipruto(aliyekuwa kijana wa umri wa miaka 19 tu) alishinda medali ya fedha katika Mbio ya Olimpiki ya 2004 katika mbio ya 3000m kuruka viunzi. Katika Mbio ya Mabingwa ya Dunia ya 2005 mjini Helsinki alishinda medali ya shaba katika mbio iyo hiyo ya 3000m. Yeye alimaliza katika nafasi ya tatu tena katika Mbio ya Dunia ya IAAF ya 2005. Katika mwaka wa 2006,alimaliza katika nafasi ya 6 katika fainali ya Mbio ya Dunia,huku akirudia nafasi yake ya 2004.

Katika mwaka wa 2007, yeye alishinda medali ya dhahabu katika mbio ya kuruka viunzi katika Mbio ya Ubingwa,Osaka. Baada ya kuhitimu timu ya Olimpiki ya 2008, kIpruto alishinda medali ya dhahabu katika mbio hiyo. Ingawa katika Mbio ya Mabingwa ya 2009, bingwa mtetezi alikuwa nambari 7 tu.

Hivi sasa anaishi Korkitony na hufanya mazoezi na kundi la Global Sports, Kaptagat karibu na Eldoret chini ya kocha Patrick Sang na Joseph Chelimo.

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Matokeo katika mashindano[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Shindano Pahala palipokimbiwa Tokeo Maelezo ya ziada
2001 Mbio ya Vijana ya Dunia Debrecen, Hungaria 2 2000 m kuruka viunzi
2003 Mbio ya Vijana ya Afrika Garoua, Kamerun 2 3000 m kuruka viunzi
2004 Mbio ya Vijana ya Dunia Grosetto, Uitalia 3 1500m
Olimpiki 2004 Athens, Ugiriki 2 3000m kuruka viunzi
Mbio ya Vijana ya IAAF Monte Carlo, Monaco 6 3000 m kuruka viunzi
2005 Mbio ya Vijana ya IAAF St Etienne, Ufaransa 37 Mbio fupi
Mbio ya Mabingwa Helsinki, Finland 3 3000m ya kuruka viunzi
Mbio ya Dunia ya IAAF Monte Carlo, Monaco 3 3000 m kuruka viunzi
2006 Mbio ya Dunia ya IAAF Fukuoka, Ujapani 18 Mbio fupi
Mbio ya Dunia ya IAAF Stuttgart, Ujerumani 6 3000 m kuruka viunzi
2007 Mbio ya Dunia ya Mabingwa Osaka, Ujapani 1 3000m kuruka viunzi
Mbio ya Dunia ya IAAF ya Fainali Stuttgart, Ujerumani 3 3000 m kuruka viunzi
2008 Olimpiki ya 2008 Beijing, Uchina 1 3000m kuruka viunzi
Mbio ya Dunia ya IAAF ya Fainali Stuttgart, Ujerumani 9 3000 m kuruka viunzi
2009 Mbio ya Dunia ya Mabingwa Berlin, Ujerumani 7 3000m kuruka viunzi
Mbio ya Dunia ya IAAF ya Fainali Thessaloniki, Ugiriki 6 3000 m kuruka viunzi

Muda bora(wa kibinafsi)[hariri | hariri chanzo]

  • 1500m - 3:35.23 (2006)
  • 3000m - 7:47.33 (2006)
  • 2000m - 5:36.81 (2001)
  • 3000m - 8:02.89 (2007)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]