Nenda kwa yaliyomo

Brahmagupta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Brahmagupta

Brahmagupta (Kisanskrit: ब्रह्मगुप्त)) (597668 BK) alikuwa Mhindi mtaalamu wa Hisabati na astronomia anayekumbukwa kwa maandishi yake kuhusu fani hizo mbili.

Alikuwa msimamizi wa paoneaanga mjini Ujjain (Madhya Pradesh).

Brahmagupta alikuwa mwanahisabati wa kwanza anayejulikana kutunga sheria za kupiga hesabu kwa kutumia sifuri. Alitunga pia sheria za hesabu kwa namba hasi.

Katika fani ya astronomia alipinga mafundisho ya siku zake kuwa dunia ni tambarare akasisitiza ni tufe. Pia alipinga mafundisho kuwa mwezi uko mbali kuliko jua akaonyesha kuwa sharti mwezi uwe karibu zaidi.