Bodi ya sakiti iliyochapishwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bodi ya saketi yenye mashimo na vifaa, pande zote mbili
Bodi ya saketi iliyochapishwa, bila vifaa

Bodi ya saketi iliyochapishwa (en:Printed circuit board - PCB) ni bodi inayotumika kwa kuunganisha vifaa vya kielektroniki kama vile transista na vingine. Pia inajulikana kama ubao wa waya zilizochapishwa ama "Printed wiring board (PWB)".

Bodi hizi kwa kawaida ni bapa la plastiki au karatasi imara au mata nyingini isiyopitisha umeme. Juu yake kuna njia nyembamba za kupitisha umeme zinazochapishwa.

Baadaye transista na vifaa vingine vinawekwa kwenye nafasi zilizoandaliwa na kufungwa kwa njia ya kulehemu (soldering). Zamani bodi ilikuwa na mashimo kwa kuweka vifaa, siku hizi teknolojia hii inatumiwa kwa vifaa vikubwa tu au kama ni bodi chache tu zinazotengenezwa. Siku hizi vifaa vinafungwa juu ya bodi tu na hii inapunguza ukubwa kwa bodi. Kazi hii inatekelezwa kwa jumla hasa kwa mashine maana vifaa vimekuwa vidogo mno.

Bodi za saketi zinatengenezwa kirahisi na siku hizi zinapatikana katika kila kifaa cha umeme kama ni tochi, simu, friji, pampu au kompyuta.

Bodi za saketi hupangwa kwa njia maalumu kwa kila kifaa na kila kazi. Siku hizi huchorwa kwa kutumia programu za kompyuta kama CAD.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mvumbuzi wa Bodi za saketi zilizochapisha aliejulikana kwa jina la Paul Eisler (1907-1995) aliyekuwa raia wa Austria, pindi alipokuwa akifanya kazi nchini Uingereza, alipoifanya moja ya circa 1936 kama sehemu ya redio. Mnamo miaka ya 1943 Marekani ilianza kutumia teknolojia ya juu kwa kiasi kikubwa kuzalisha redio zilizotumika katka vita kuu ya pili ya dunia. Baada ya vita, kunako miaka ya 1948, teknolojia hiyo ilitolewa kwa ajili ya matumizi ya kibiashara katikati ya miaka ya 1950, baada ya mchakato Jotoridi Sembly ilitengenezwa na Jeshi la Marekani.