Bodi ya saketi iliyochapishwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bodi ya saketi yenye mashimo na vifaa, pande zote mbili.
Bodi ya saketi iliyochapishwa, bila vifaa.

Bodi ya saketi iliyochapishwa (kwa Kiingereza: en:Printed circuit board - PCB; pia inajulikana kama ubao wa nyaya zilizochapishwa ama printed wiring board (PWB)) ni bodi inayotumika kwa kuunganisha vifaa vya kielektroniki kama vile transista na vingine.

Bodi hizo kwa kawaida ni bapa la plastiki au karatasi imara au mata nyingine isiyopitisha umeme. Juu yake kuna njia nyembamba za kupitishia umeme zinazochapishwa.

Baadaye transista na vifaa vingine vinawekwa kwenye nafasi zilizoandaliwa na kufungwa kwa njia ya kulehemu (soldering). Zamani bodi ilikuwa na mashimo kwa kuweka vifaa, siku hizi teknolojia hii inatumiwa kwa vifaa vikubwa tu au kama ni bodi chache tu zinazotengenezwa. Siku hizi vifaa vinafungwa juu ya bodi tu na hii inapunguza ukubwa kwa bodi. Kazi hii inatekelezwa kwa jumla hasa kwa mashine maana vifaa vimekuwa vidogo mno.

Bodi za saketi zinatengenezwa kirahisi na siku hizi zinapatikana katika kila kifaa cha umeme kama ni tochi, simu, friji, pampu au kompyuta.

Bodi za saketi hupangwa kwa njia maalumu kwa kila kifaa na kila kazi. Siku hizi huchorwa kwa kutumia programu za kompyuta kama CAD.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mvumbuzi wa Bodi za saketi zilizochapisha, aliyejulikana kwa jina la Paul Eisler (1907-1995) aliyekuwa raia wa Austria, pindi alipokuwa akifanya kazi nchini Uingereza, alipoifanya moja ya 1936 hivi kama sehemu ya redio.

Mnamo mwaka 1943 Marekani ilianza kutumia teknolojia ya juu kwa kiasi kikubwa kuzalisha redio zilizotumika katika vita kuu ya pili ya dunia. Baada ya vita teknolojia hiyo ilitolewa kwa ajili ya matumizi ya kibiashara katikati ya miaka ya 1950, baada ya mchakato Jotoridi Sembly ilitengenezwa na Jeshi la Marekani.

Utengenezaji[hariri | hariri chanzo]

Bodi iliyochapishwa ni kiunganishi kikubwa baina ya saketi moja na nyingine kwa muunganiko wa nyaya zinazosambaza umeme au taarifa za elektroniki. Bodi hii ni muhimu sana na hutengenezwa kwa wingi na viwanda ila hivi sasa utengenezwaji wake umerahisishwa na kufanya upatikanaji wake kuwa rahisi zaidi.

Mahitaji[hariri | hariri chanzo]

Programu maalumu ya kutengeneza muonekano wa saketi yako ikiwa imekamilika kwa muonekano wa picha kabla ya kutengenezwa. Pia utahitaji pasi ya umeme inayotumika kwa matumizi ya kawaida ya nyumbani. Mashine ya kuchapisha nakala kutoka kwenye kompyuta (printa), mashine ya kutobolea bodi, bakuli la maji, karatasi maalumu itakayotumika kuhamisha mchoro na mwisho kabisa bodi itakayotumika kutengezea mchoro.

Hatua za kutengeneza[hariri | hariri chanzo]

1. Kwanza kabisa andaa mchoro wako kwenye kompyuta yako kwa umakini na hakikiisha ndicho unachotaka kutengenezea bodi ya kitu unachotaka kukitengeneza.

2. Kisha chukua karatasi maalum utakayoitumia kuhamishia mchoro wakko wa sakiti kwa kutengezea bodi ya sakiti iliyochapishwa.

3. Kisha toa nakala ya mchoro wako kupitia karatasi maalum iliyoelezewa kwenye hatua iliiyopita(hatua ya pili) kwa kutumia mashine maalum ya kutoa nakala toka kwenye kompyuta.

4. Bandika karatasi yako kwenye bodi unayotaka kutengenezea sakiti iliiyochapishwa na baada ya hapo piga pasi bodi yako ikiwa pamoja na karatasi haalu iliyochapiswa mchoro wa sakiti kwa moto wa wastanii ilikuepuka kuunguza.

5. Mara baada ya hapo loweka bodi yako kwenye maji ya baridi ya wastani il ikuweza kulainisha karatasi iliyobandikwa kurahisisha utoaji wake. Mara inapokuwa tayari toa karasi uliyoibandika kwenye ubao wako kisha safisha ubao wako.

6. Mwisho chukua ubao wako na kuuweka kwenye mashine ya kutobolea na kutoboa matundu sahihi katika ubao wako.

7. Mpaka hapo ubao wako wa saikiti iliyochapishwa utakuwa tayari kwa matumizi ya kutengenezea kifaa chako cha elektroniki.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.