Bice Osei Kuffour
Bice Osei Kuffour | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 17 Novemba 1981 |
Nchi | Ghana |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Bice Osei Kuffour (alizaliwa 17 Novemba ,1981) ni mwanamuziki wa hiplife wa nchini Ghana, anayejulikana kwa jina la Obour, ambalo linamaanisha "jiwe" katika lugha ya Kiakan . Alikua Rais wa Muungano wa Wanamuziki wa Ghana, [1] katika kundi la umbrella group ambalo linaunganisha wanamuziki wote nchini Ghana bila kujali aina ya muziki. [2] Bice Osei Kuffour alishiriki uchaguzi wa mchujo wa NPP katika eneo la bunge la Asante Akyem Kusini kama mgombea ubunge. Baadae aliteuliwa kuwa katibu wa kamati ya Matangazo ya kampeni ya NPP 2020. Obour ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ghana, Ni mwanaharakati wa kijamii ambaye ni balozi wa kitaifa wa usalama barabarani; Balozi wa WHO wa Kifua Kikuu Baraza la Uingereza & Tume ya Misitu ya Ghana na Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi. Pia ni rais na Mwanzilishi wa shirika la Christiana Addo Memorial Foundation ambalo linakuza elimu, usafi wa mazingira, usafi wa kibinafsi na uwezeshaji wa vijana huko Asante Akyem.[3]
Maisha na kazi
[hariri | hariri chanzo]Obour alizaliwa "Braha Bebu Me" (Dekyemenso) katika Mkoa wa Ashanti mnamo 7 Novemba 1981, na Christiana Addo na Mchungaji BO Kuffour. Akiwa na umri wa miaka sita, Obour alicheza ngoma za aina nyingi, hasa Atumpan, katika jumba la chifu la Juaso-Ashanti Akyem ambako baba yake alikuwa akiongoza. Obour alisoma katika mbalimbali kama Shule ya Majaribio ya Jimbo ( Kumasi ), Shule ya Kliniki ya Soul ( Accra ), Shule ya Sekondari ya Garison Junior ( Kambi ya Burma ) na Shule ya Mfantsipim ( Cape Coast ).
Baada ya kumaliza shule ya upili, Obour aliomba usaidizi kutoka kwa binamu yake aliyeishi London, J. Amano, ambaye alimuunganisha na lebo yake ya binafsi ya Soul Records. Baadae alitoa wimbo wa Atentenben ambao ulishinda tuzo tatu za Soul Records kwenye tuzo za muziki za Ghana (Ghana Music Awards) mnamo 2002, pamoja na Video ya mwaka. Nyimbo hizi, na zingine za lebo hiyo, zilipelekea Soul Records kutunukiwa kama Record Lebo bora ya Mwaka. Video hiyohiyo ilishinda tuzo bora zaidi katika tuzo za muziki za Our Music Awards (OMA) mnamo 2002.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Obour Elected MUSIGA President". www.modernghana.com. Iliwekwa mnamo 19 Agosti 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Selase Attah, "Pressure mounts on Obour as MUSIGA elections loom" Ilihifadhiwa 24 Julai 2015 kwenye Wayback Machine., Ghanaie.com, 12 June 2015.
- ↑ https://mobile.ghanaweb.com/person/Bice-Osei-Kuffour-338
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bice Osei Kuffour kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |