Nenda kwa yaliyomo

Bert Cameron

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bertland "Bert" Cameron (alizaliwa 16 Novemba 1959) ni mwanariadha mstaafu wa Jamaika ambaye alishiririki zaidi katika mbio za mita 400. Aliwakilisha Jamaika katika matoleo matatu mfululizo katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto. Cameron alishinda taji la mita 400 katika Mashindano ya kwanza ya Dunia katika Riadha. Pia alikuwa bingwa wa Michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 1982 [1] katika hafla hiyo na alishinda idadi ya medali za dhahabu katika mashindano ya kikanda. Alisaidia wanariadha wa Jamaika kupata medali ya fedha katika mbio za kupokezana za mita 4×400 kwenye Olimpiki ya Seoul mwaka 1988.

Cameron alibeba bendera ya Jamaika katika sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto mwaka 1984 huko Los Angeles, California. Alichaguliwa kama Mwanaspoti bora wa mwaka wa Jamaika mara tatu mfululizo kutoka mwaka 1981 hadi 1983. [2] Kwa sasa ni kocha nchini Jamaika.

  1. "Commonwealth Games Federation - Our People".
  2. Foster, Anthony (2009-11-13). Bert Cameron no longer with Wolmer's - But coach insists he was not forced out Archived 17 Novemba 2009 at the Wayback Machine. The Jamaica Star. Retrieved on 2010-11-07.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bert Cameron kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.