Benki ya Wanawake Tanzania
Benki ya wanawake Tanzania (kwa Kiingereza: Tanzania Women Bank Limited; kifupi: TWBL) ni benki ya Tanzania ambayo ina utaalamu katika kutoa huduma za kifedha kwa wanawake. Imeorodheshwa kama "Taasisi ya Fedha iliyosajiliwa" na Benki Kuu ya Tanzania, mdhibiti wa benki za taifa.[1]
Benki hii ni taasisi ndogo ya kifedha nchini Tanzania, ambapo usawa wa wanahisa wa benki hiyo ulikuwa na thamani ya TSh8.5 bilioni (takriban dola milioni 4 za Kimarekani).[2]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wazo la kuanzisha Benki ya Wanawake nchini Tanzania lilianza mnamo mwaka 1999, wakati wajasiriamali kadhaa wa kike walipomwendea Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin William Mkapa, na wazo hilo. Baada ya miaka nane, mnamo mwaka 2007, Benki ya Wanawake Tanzania iliundwa. Benki ilifunguliwa rasmi kwa biashara mnamo Julai 28, mwaka 2009. Lengo la TWB ni kuwawezesha wanawake kiuchumi na kijamii. Benki hii inatumika kwa jamii zote ikiwa ni pamoja na wenye kipato cha chini, mashirika makubwa na biashara ndogo na za kati (SMEs).[3]
Mtandao wa matawi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Novemba mwaka 2014, benki hii ilikua na matawi katika maeneo yafuatayo:[4]
- Tawi la Mkwepu - Jengo la Posta ya Zamani, Mtaa wa Mkwepu, Dar es Salaam
- Tawi la Kariakoo - Mtaa wa Aggrey Likoma, Dar es Salaam
- Tawi la Dodoma - Jengo la Posta / TTCL, Barabara ya Reli, Dodoma
- Tawi la Mwanza - Jengo la Ofisi ya Zamani, Barabara ya Posta, Mwanza
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Website of Bank of Tanzania Ilihifadhiwa 6 Novemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Partial List of Licensed Commercial Banks In Tanzania
- Tanzania Women's Bank To List On DSE In 2012
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ BOT, . "Directory of Financial Institutions Operating in Tanzania". Bank of Tanzania (BOT). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-19. Iliwekwa mnamo 22 Novemba 2014.
{{cite web}}
:|first=
has numeric name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ TDN (29 Januari 2016). "Tanzania: Women's Bank for Expansion". Tanzania Daily News (TDN) via AllAfrica.com. Dar es Salaam. Iliwekwa mnamo 31 Januari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ TWB, . "Tanzania Women's Bank History". Tanzania Women's Bank (TWB). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-16. Iliwekwa mnamo 22 Novemba 2014.
{{cite web}}
:|first=
has numeric name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ TWB, . "The Branches of Tanzania Women's Bank". Tanzania Women's Bank (TWB). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-29. Iliwekwa mnamo 22 Novemba 2014.
{{cite web}}
:|first=
has numeric name (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Benki ya Wanawake Tanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |