Baby Madaha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Baby Madaha
Amezaliwa Baby Joseph Madaha
19 Novemba 1988 (1988-11-19) (umri 31)
Utaifa Mtanzania
Kazi yake Muigizaji, msanii wa muziki wa kizazi kipya,
Miaka ya kazi 2000-hadi sasa

Baby Madaha (alizaliwa jijini Mwanza 19 Novemba 1988) ni mwanamke aliyejikita katika tasnia ya filamu za Kitanzania pamoja na muziki.

Mwanadada huyu alijishindia tuzo maarufu nchini Tanzania ya BSS- Bongo Star Search mwaka 2007.

Baby Madaha ametamba zaidi na kibao chake cha Amore[1].

Mwaka 2013 alisaini mkataba na lebo ya muziki nchini Kenya iitwayo Candy n Candy[2].

Katika tasnia ya filamu amejulikana sana kwa filamu iitwayo Nani ambayo ilimpatia tuzo huko Ujerumani.

Baadhi ya tamthilia alizowahi kucheza ni

  • Blessed by God
  • Tifu la mwaka [3]
  • Misukosuko
  • Ray of hope

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Biofilm.png Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Baby Madaha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.