Ayi Kwei Armah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ayi Kwei Armah (amezaliwa 1939) ni mwandishi maarufu kutoka nchi ya Ghana.[1]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa na wazazi waliozungumza lugha ya Kifante, huku upande wa babake, Armah, ukiwa na mababu wa familia ya kifalme wa kabila la Ga katika mji wa bandari ya Sekondi-Takoradi, Ghana.

Armah, baada ya kusoma katika shule ya Achimota, alihama Ghana mwaka wa 1959 kusomea katika shule ya Groton, Massachusetts. Baada ya kupata shahada yake, alijiunga na Chuo Kikuu cha Harvard, huku akipata shahada ya elimu ya jamii.

Baada ya hapo alihamia nchi ya Aljeria na kufanya kazi kama mtafsiri wa jarida la Révolution Africaine.

Mnamo mwaka wa 1964, Armah alirudi Ghana, ambapo alikuwa mwandishi wa Runinga ya Ghana na baadaye alifunza Kiingereza katika shule ya Navrongo.

Kati ya mwaka wa 1967 na 1968, alikuwa mhariri wa jarida la Jeune Afrique, magazine mjini Paris.

Kati ya mwaka wa 1968 na 1970, Armah alisoma katika Chuo Kikuu cha Colombia, huku akipata shahada nyingine ya uandishi bunifu. Katika miaka ya 1970, alifanya kazi kama mwalimu katika eneo la Afrika Mashariki, katika taasisi ya Elimu ya Kitaifa, Chang'ombe, Tanzania, na katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Lesotho.

Aliishi katika mji wa Dakar, Senegal, katika miaka ya 1980 na alifunza katika Taasisi ya Amherst na Chuo Kikuu cha Wisconsin–Madison.

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Katika Fragments (Chembechembe) (1971), mhusika mkuu, Baako, ni mtu aliyetembea kote. Ametembea hadi nchi ya Marekani na kupata elimu yake huko. Lakini nchini Ghana anatazamwa na mshangao na heshima kama daraja la maisha ya Magharibi. Nyanyake Baako, Naana, mpiga ramli ambaye ni kipofu, anaweza kuwasiliana na waliokufa. Kwa kushindwa kutimiza yote ambayo watu wanatarajia atomize Baako anavunjika. Kama tu katika riwaya yake ya kwanza, Armah anatofautisha Dunia mbili za vitu na maadili, ufisadi na ndoto, Dunia mbili za uwajibikaji na shinikizo la kijamii.

Why Are We So Blest? (Mbona Tukabarikiwa Kiasi Hiki?) (1972) ina muktadha wake katika chuo ikuu cha Marekani, na mwanafunzi mwenye bidii, Modin Dofu, amewacha masomo yake katika Chuo Kikuu cha Harvad. Huku akiwa amekengeushwa akili yake imegawanywa kati ya uhuru na mitazamo ya Kimagharibi. Anakutana na mwanamke mweusi wa Kiportugal anayeitwa Solo, ambaye tayari amerukwa na kichwa, na mwanamke mweupe wa Kimarekani, Aimée Reitsch. Solo, mwandishi aliyekataliwa, anaandika kumbukumbu, ambayo ndiyo msingi wa riwaya yake. Tabia ya Aimée ya kutotangamana na watu na kujitolea kwake katika mapinduzi mwishowe kunasababisha maangamizi, ambapo Modin anwawa jangwani na Wanamapinduzi wa O.A.S.

Si waandishi wengi wa Kiafrika ambao wameandika kuhusu biashara ya watumwa siku za zamani.[onesha uthibitisho] Hata hivyo, mada hii inaangaziwa na Armah katika kitabu cha Two Thousand Seasons (Misimu Laki Mbili) (1973), utendi, ambapo sauti ya kijamii inaongea kupitia historia ya Afrika, misimu yake ya mvua na kiangazi, kutoka kipindi cha miaka laki moja. Wakandamizaji wa Kiarabu na wa Ulaya wanaonyeshwa kama "wawindaji" na "waharibifu". Riwaya hiyo inaandikwa kwa sauti ambayo ni kana kwamba inajaribu kupata mafunzo ya maana, na inabadilika kutoka hadithi za kweli na za kuhusu maisha ya Kwei Armah hadi kutafakari kwa kifalsafa ambao kunaotabiri ujio wa enzi mpya.

The Healers (Waponyaji) (1979) ilichanganya ukweli na ubunifu kuhusu kuanguka kwa Dola maarufu a Ashanti. Waponyaji katika riwaya hiyo ni madaktari wa matibabu ya kienyeji wanaoona kusambaratika kama ugonjwa wenye uwezo wa kusababisha maafa mengi Barani Afrika.

Armah alibaki kimya kama mwandishi wa riwaya kwa kipindi kirefu hadi mwaka wa 1995 alipochapisha kitabu cha Osiris Rising (Osiris Akiinuka), kilichoonyesha kikundi cha siasa kali cha mapinduzi ya kielimu, kinachofanya Misri ya kale kuwa kituo cha mafunzo yake.

Armah mara nyingi ametazamwa kama mmoja wa kizazi kipya cha Waandishi wa Afrika baada ya Chinua Achebe na Wole Soyinka.[onesha uthibitisho] Wakati uo huo yeye ametazamwa kama ishara ya "kipindi cha kukata tamaa." Hasa maandiko ya baadaye ya Armah yameibua hisia kali kutoka kwa wakosoaji. Two Thousand Seasons (Misimu Laki Mbili) imetazamwa na wachache kuwa vuguvugu na yenye maneno mengi kupita kiasi, ingawa Wole Soyinka aliona mtazamo wake kama wa Kidunia na wa Kibinadamu.

Kama mwandishi wa insha Armah amepambana na kujitambua na shida ya Afrika. Anajali sana kuhusu kutengeneza shirika la Waafrika wote Duniani litakalojumuisha tamaduni mbalimbali na lugha katika Bara Afrika. Armah ameomba lugha ya Kiswahili itumike kama lugha rasmi ya Bara la Afrika.

Baadhi ya vitabu[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ayi Kwei Armah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.