Aspreno wa Napoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Luca Giordano, Watakatifu wasimamizi wa Napoli, mmojawao akiwa Aspreno, mbele ya Yesu Msulubiwa, XVII seculo, Palazzo Reale, Napoli, Italia.

Aspreno wa Napoli alikuwa Mkristo wa karne ya 1 BK; anatajwa kama askofu wa kwanza wa mji huo wa Italia Kusini[1].

Asili yake haijulikani.

Inasemekana aliinjilishwa na Mtume Petro alipokuwa akielekea Roma.

Baadaye akawa askofu kwa miaka 23, akistawisha Kanisa la Napoli.

Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Agosti[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.