Nenda kwa yaliyomo

Asiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Asiti
Asiti mweusi
Asiti mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Eurylaimoidea (Ndege kama vijogoo-shamba)
Familia: Philepittidae (Ndege walio na mnasaba na asiti)
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 4:

Asiti (kutoka Kimalagasi: asity) ni ndege wadogo wa familia Philepittidae. Wanatokea misitu ya Madagaska. Manyoya ya madume ni meusi na/au buluu na spishi mbili zina tumbo njano. Wana ngozi tupu kuzunguka macho yenye rangi ya buluu au majani. Majike wana rangi ya kahawa au majivu. Spishi za Neodrepanis zina domo lililopindika kama lile la chozi. Asiti wana mkia mfupi na ulimi uliogawanyika sehemu mbili. Hula matunda hasa lakini mbochi pia na pengine wadudu. Tago lao limefumika kwa manyasi, vitawi na nyuzinyuzi na lina umbo wa parachichi. Jike huyataga mayai 2-3.

Makala hii kuhusu "Asiti" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili asity kutoka lugha ya Kimalagasi. Neno (au maneno) la jaribio ni asiti.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.