Asidi boriki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Asidi boriki ni asidi ya boroni yenye fomula ya H3BO3. Asidi boriki hutumiwa kama dawa ya kipukusi. Inaweza pia kutumika kama dawa ya kuhifadhi kuoza (E 284). Asidi boriki hupatikana wakati wa kutengeneza kioo na kauri.

Hutumika katika ujenzi kama kizuizi cha moto. Ikiyeyushwa katika maji, husaidia kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia.

Asidi boriki ni sumu. Uharibifu hufanywa kutokana na kumeza karibu mg 50 kwa kilo ya uzito wa mwili.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asidi boriki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.