Arsasi wa Nikomedia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Arsasi wa Nikomedia (alifariki Nikomedia, leo Izmit, nchini Uturuki, 24 Agosti 358) alikuwa askari wa Dola la Roma mwenye asili ya Persia.

Baada ya kuungama hadharani imani ya Kikristo wakati wa kaisari Licinius, aliacha jeshi aende kuishi upwekeni karibu na Nikomedia.

Alihimiza wakazi wa mji huo kusali na kufanya toba akitabiri tetemeko la ardhi lililouangamiza pamoja na kumuua mwenyewe[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Agosti.[2]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/66170
  2. Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 2001, ISBN|88-209-7210-7)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.