Nenda kwa yaliyomo

Alvin and the Chipmunks

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alvin and the Chipmunks
Imeongozwa na Tim Hill
Imetayarishwa na Janice Karman
Ross Bagdasarian, Jr.
Imetungwa na Jon Vitti
Will McRobb
Chris Viscardi
Nyota Jason Lee
David Cross
Cameron Richardson
Jane Lynch
Justin Long
Matthew Gray Gubler
Jesse McCartney
Muziki na Christopher Lennertz
Imehaririwa na Peter Berger
Imesambazwa na 20th Century Fox
Imetolewa tar. Desemba 14, 2007 (2007-12-14)
Ina muda wa dk. Dakika 91
Nchi United States
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu $60,000,000
Mapato yote ya filamu $361,336,633
Ikafuatiwa na Alvin and the Chipmunks: The Squeakquel (2009)

Alvin and the Chipmunks ni filamu ya vichekesho-muziki ya mwaka wa 2007 kutoka nchini Marekani. Filamu inachanganya wahusika hai na katuni. Filamu ipo katika msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Ndani yake anakuja Jason Lee, David Cross, Cameron Richardson, Jane Lynch na sauti zimeingizwa na Justin Long, Matthew Gray Gubler na Jesse McCartney. Filamu inawashirikisha kina Alvin and the Chipmunks na inatokana na mfululizo wake wa TV ambao ni katuni na una jina-sawa-na hili la filamu. Filamu imeongozwa na Tim Hill, imesambazwa na 20th Century Fox na kutayarishwa na Regency Enterprises na Bagdasarian Productions.

Filamu ilijongewa mno na watahakiki ikiwa moja kati ya picha mbaya kuliko ya mwaka lakini ilipata mafanikio makubwa kifedha: kwa bajeti ya dola milioni $55-$60, na imeingiza kiasi cha milioni $217 huko Amerika ya Kaskazini na kiasi cha milioni $361 kwenye box office ya dunia nzima,[1] na ilikuwa filamu ya saba-kwa-mauzo bora ya DVD kwa mwaka wa 2008, kwa kupata kiasi cha zaidi ya milioni $101.

Hadithi inaanza nyuma ya kilima, kilichopo kwenye msitu wakati wa kipindi cha baridi. Mti ambao kina chipmunks Alvin (imetiwa sauti na Justin Long), Simon (imetiwa sauti na Matthew Gray Gubler), na Theodore (imetiwa sauti na Jesse McCartney) wanaishi unakatwa na kuchukuliwa na gari hadi huko mjini Los Angeles na kuwa mti wa Krismasi.

Wakiwa mjini LA, kina Chipmunks wanakutana na mtunzi wa nyimbo anayehaha David Seville (Jason Lee) ambaye alikuwa na wimbo wake mpya ambao umekataliwa na mkurugenzi mtendaji wa JETT Records, Ian Hawke (David Cross) ambaye zamani alikuwa akiishi pamoja na Dave wakati wapo chuo. Dave awali alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na jirani yake, Claire Wilson (Cameron Richardson). Ameachana naye kwa sababu alihisi ya kwamba yupo na kazi tele, hamjali na wala hana muda wa kuwa na yeye.

Baada ya kuvurunda mahojiano ya Dave, kina Chipmunks wakajirusha ndani ya kikapu na kumfuata Dave hadi nyumbani kwake. Pindi walipofika nyumbani, Dave kagundua kina Chipmunks, na kwa bahati mbaya akagongwa kichwani na kupoteza fahamu. Baada ya kuamka, kawatupa nje hadi hapo alipowasikia wakiimba wimbo wa "Only You (And You Alone)".

Dave kisha anaingia nao mkataba; waimbe nyimbo anazotunga, kwa malipo ya chakula na malazi kwa ajili yao. Hata hivyo, yote hayakwenda vyema, kwa vile uwakilishi wa kazi ya Dave umeharibiwa na virangi-rangi vyake, na pale Alvin anapojaribu kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya chakula cha jioni na Claire, mambo yamekuwa mabaya mno na matokeo yake kamkataa baada ya Dave kumwambia Claire kwamba "Maisha yangu yamehujumiwa na chipmunks wanaoongea". Ili kuweka sawa kwa Dave, Alvin, Simon, na Theodore wanaenda kwa Ian kwa jaribio la kutaka kurekodi wimbo na kuingia mkataba na studio.

Pindi kina Chipmunks walipoimba wimbo wa Dave kwa Ian, Ian akaingia nao mkataba na kumkodi upya Dave kwa siku nyingine. Baada ya single kadhaa, kina Chipmunks wakawa maarufu kupindukia. Pale Dave anapoelezea wasiwasi wake kwa ajili ya usalama wao na kusisitiza kwamba kina Chipmunks ni "watoto" ambao hawa-hitaji kuchizika katika maisha yao, Ian anawashawishi kina Chipmunks kwamba Dave anawarudisha nyuma.

Hatimaye, Dave na Chipmunks wanamabishano na, kukasirikiana, Dave anawaambia kama wanampenda "Mjomba Ian" sana, basi waende kuishi naye. Wamevutiwa sana na Ian kwa mara ya kwanza, lakini pindi walipoweka sawa ziara za pwani-kwa-pwani, Ian anajipatia faida kwa ujinga wao, kwa kubadilisha taswira yao na kuwafanyisha mikazi kupitiliza. Muda huohuo, Dave ana-hamu na kina Chipmunks na anatamani wangerudi nyumbani. Anampigia simu Ian kuangalia kama ataweza kuzungumza nao lakini Ian anakataa, halafu anaficha shauku ya Dave kwa vijana wale.

Baadaye, kina Chipmunks wanavua mavazi, na habari zikaenea katika vyombo vya habari vyote. Dave, amechukizwa na kile Ian alichofanya kwa vija wale, na kuamua kuchukua hatua mikononi mwake kwa kujiingiza kwenye tamasha lao lililokuwa likifanyika katika ukumbi wa Los Angeles Orpheum Theater.

Kabla ya tamasha kubwa, daktari anasema kwamba kina Chipmunks hawawezi kuimba kwa sababu sauti zao zimekauka. Ian anakataa kulipa hela za watu alizochukua kwa ajili ya tamasha na kuwaamuru kina Chipmunks wainue mdomo tu. Kwa msaada wa Claire, Dave kaingia kwenye tamasha kwa njia za panya, lakini akadakwa na mmoja kati ya walinzi wa usalama. Wakati kina Chipmunks wanamwona Dave anatolewa nje, wanagundua kama walikuwa wakichezewa mchezo, wakaamua kwamba wametosheka na Ian, wakaanza fujo na kuvuruga kila kitu kwenye tamasha.

Punde waka-kamatwa na Ian wakati Dave anajaribu kuwaokoa. Akawafungua kwenye banda na kujiandaa kuwachukua na kwenda nao mjini Paris. Dave kajaribu kumshawishi Ian awaache vijana lakini Ian kakataa. Ian kisha akaingia kwenye limo lake na vijana na Dave kawakimbiza lakini vijana tayari walikuwa wameshatorokea kwenye gari la Dave. Dave ghafula akaminya breki na kukubali kwamba anawapenda kama familia moja. Muda huohuo, Ian anatazama kwenye sanduku na kushtushwa kuona vijana wamejibadilisha wenyewe na kuweka mdoli unaongea.

Wakati fulani baadaye, wakati vijana wamekubaliwa rasmi kuwa familia moja, wamemwalika tena Claire kwa ajili chakula cha usiku. Alvin akasababisha ajali ya shoti ya saketi pindi alipokuwa akijaribu kufungua chupa ya shampeni. Dave anajaribu kutosema lolote, lakini shoti ya saketi imesababisha kiza ndani. Dave akasema kwa kushikilia muda, kwa zogo kubwa "ALLLLVINNN!!", ambapo Alvin anajibu na "Okay!".

Washiriki

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]