Justin Long
Justin Long | |
---|---|
Amezaliwa | Justin Jacob Long[1] 2 Juni 1978 Fairfield, Connecticut, Marekani |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1999–present |
Justin Jacob Long (amezaliwa tar. 2 Juni 1978) ni mwigizaji wa filamu na vipindi vya televisheni kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa nyusika zake za kwenye filamu za Hollywood kama vile Galaxy Quest, Jeepers Creepers, Dodgeball, Waiting..., Accepted, Live Free or Die Hard, He's Just Not That into You, Drag Me to Hell, na Youth in Revolt, Alpha and Omega, na tashihisi yake ya Mac kwenye kampeni za matangazo ya Apple ya "Get a Mac".
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Long alizaliwa mjini Fairfield, Connecticut. Baba yake, R. James Long, alikuwa mwanafalsafa na profesa wa Kilatini katika Chuo Kikuu cha Fairfield, na mama yake, Wendy Lesniak,[2] mwigizaji ambaye ameigiza zaidi kwenye majukaa. Long amekulia katika makuzi ya Romani Katoliki.[3] Bibi yake ni Msicili.[4] Kaka yake mkubwa, Damian, ni mwigizaji mtaani vile vile mwalimu na mwongozaji wa tamthilia kwenye shule ya Weston High School. Ndugu yake mdogo, Christian, ameonekana kwenye filamu ya ndugu yake Accepted kama mleta bahati wa shule. Long amehitimu kwenye shule ya Fairfield College Preparatory School, shule ya Jumuiya ya Yesu, na Vassar College, ambapo alikuwa mchekeshaji kwenye moja ya kundi lililoitwa Laughingstock na kushiriki kwenye michezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Butterflies Are Free. Ameacha chuo mapema ili ajiendeleze zaidi na shughuli za uigizaji. Kabla ya kuacha, Long alifanyakazi katika chuo Kikuu cha Sacred Heart mjini Fairfield, Connecticut, akiwa kama mwelekezi/mashauri ya kikundi cha watoto.
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Justin Long Bio". Young Hollywood. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-21. Iliwekwa mnamo 2010-08-30.
- ↑ "Justin Long Interview, Die Hard 4 - MoviesOnline". Moviesonline.ca. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-09-06. Iliwekwa mnamo 2010-03-22.
- ↑ Topel, Fred (2006-08-14). "Interview: Justin Long". Cinema Blend. Iliwekwa mnamo 2010-03-22.
My family is Roman Catholic and kind of conservative...
- ↑ Murray, Rebecca. "Justin Long Talks About The Sasquatch Dumpling Gang and Strange Wilderness". About.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-18. Iliwekwa mnamo 2010-07-01.
My family is Roman Catholic and kind of conservative...
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Kigezo:IMDb
- Mac Ads
- RadarOnline Article about Apple not bringing Long back, and bringing him back after all Archived 7 Machi 2009 at the Wayback Machine.
- Interview with Justin Long at SuicideGirls.com
- Video interview with Justin Long Archived 22 Mei 2013 at the Wayback Machine. at the premiere of The Break-Up
- "Robin's Big Date Archived 5 Februari 2009 at the Wayback Machine." on Transbuddha.com