Almeda Abazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Almeda Abazi Sayişman (amezaliwa 13 Februari 1992) ni mwigizaji wa Albania, mwanamitindo, malkia wa urembo ambaye katika mashindano matatu ya urembo aliyoshiriki, alichaguliwa kama malkia na akashinda Miss Tiran, Miss Albania na Miss Globe Universe mnamo 2008. [1] Abazi alifung ndoa ana mwigizaji wa Kituruki Tolgahan Sayışman mnamo 14 Februari 2017 huko Los Angeles.

[2]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Alimaliza elimu yake ya sekondari katika Chuo cha Kibinafsi cha Tarhan huko Istanbul. Alisoma uigizaji katika chuo cha Bil Sanat Academy of Istanbul Aydın . [3] Almeda Abazi aliishi Uturuki na kuamua kuendelea na maisha yake ya kikazi nchini Uturuki. Ameonekana katika filamu ya Konak, Show Business na pia katika Tamthilia ya Uturuki inayoitwa Ayrılık .

Pia alijiunga na Yok Böyle Dans mnamo 2011 na Survivor Ünlüler-Gönüllüler . aliigiza katika Muhteşem Yüzyıl kama Valeria. Alionekana katika Para Bende na Murat Ceylan kama mtangazaji kwenye TV8 (Kituo cha TV cha Uturuki) na akajiunga na shindano la Survivor All Star tena mnamo 2015.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Almeda Abazi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Almeda Abazi". Sabah. 
  2. "Almeda Abazi". Sabah. 
  3. "Survivor Almeda Abazi Sayışman Kimdir ?" (kwa Turkish). 2012. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 March 2015. Iliwekwa mnamo 2012-04-30.  Check date values in: |archivedate= (help)