Nenda kwa yaliyomo

Alibhai Mulla Jeevanjee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Alibhai Mulla Jeevanjee
Sanamu ya Mzee Jiwanji katika bustani yenye jina lake
Amezaliwa1856
Amefariki(1856
Kazi yakemfanyabiashara


Alibhai Mulla Jeevanjee (1856-1939) alikuwa mfanyabiashara Mhindi ambaye alizaliwa Karachi iliyokuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza. Alihamia Mombasa nchini Kenya katika Afrika ya Mashariki mwaka wa 1890 baada ya kukaa Australia kwa miaka michache.[1]Alianza shughuli zake za urasirimali katika Karachi nchini Pakistan kabla ya kuhamia Afrika Mashariki. Mnamo 1895, A M Jeevanjee wa Karachi - kama alivyoitwa wakati huo, alipewa kandarasi ya kutafuta wafanyikazi na kampuni ya Imperial British East Africa iliyokuwa imepewa kandarasi ya kujenga reli.Wengi wa wafanyikazi hawa walitoka eneo la Punjab huko India. Kundi la kwanza kufika lilikuwa na jumla ya watu 350 na idadi iliongezeka kwa miaka sita ijayo na kufikia jumla ya wafanyikazi 31,895. Wengi wao walikuwa Sikhs, Wahindi na Waislamu ambao walifanya kazi kama vibarua wenye ujuzi, mafundi, waashi, maseremala, washonaji, mafundi wa mashine na waweka umeme.[2]
Baadaye alifuatilia uana biashara kwa kufungua tawi la ofisi yake Karachi katika mji wa Mombasa. Alianza kufanya biashara zingine katika mkoa huo baada ya kusimamia ujenzi wa reli. Na ilianza kusambaza vifaa ambayo ni pamoja na chakula kwa wafanyikazi hao waliokuwa wanajenga reli.Kampuni yake pia ilipewa kandarasi za kujenga ofisi za serikali, vituo vya reli na ofisi za posta.[1]

Biashara

[hariri | hariri chanzo]

Alifuatilia maslahi mbalimbali ya biashara wakati wa kuishi kwake huko Australia na hata baada ya kuhamia Afrika Mashariki.

African standard

[hariri | hariri chanzo]

Wakati ujenzi wa reli ya Kenya-Uganda ilifika ziwa Victoria, Jeevanjee alizindua Africa standard ambayo ilikuwa gazeti ya kila wiki. Alikuwa ameajiri mhariri mwandishi, W.H. Tiller ambaye kazi yake ilikuwa kusimamia shughuli za gazeti hilo.Mnamo 1905, aliuza Africa standard kwa wafanyabiashara wawili wa Uingereza ambao walibadili jina la gazeti hilo kuwa East African Standard. Baadaye mnamo 1910 gazeti hili likawa la kila siku na likahamisha makao yake makuu kutoka Mombasa hadi Nairobi ambao ulikuwa kituo cha kibiashara.[3]

Bustani ya Jeevanjee

[hariri | hariri chanzo]

Alianza kujenga Bustani ya Jeevanjee mnamo 1904 ambayo baadaye alipeana kwa watu wa Nairobi mwaka wa 1906 kama mahali pa kupumzika.[4]Bustani hiyo iligonga vichwa vya habari mwaka wa 1991 baada ya baadhi ya viongozi katika mamlaka kuwa na njama ya kegeuza bustani hiyo kuwa eneo la biashara.Kulikuwa na pendekezo la ujenzi wa egezo la ghorofa la gari. Hii ilikuwa dhidi ya matakwa ya Jeevanjee.Binti ya Jeevanjee aliyekuwa amebaki hai, marehemu Shirin Najmudean alihamia Nairobi ili kuzuia mapendeleo haya yaliyokuwa yamepangwa kwenye kipande hiki cha ardhi.[5]

Pia tazama

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 Thomas R. Metcalf (24 Aprili 2007). Imperial Connections: India in the Indian Ocean Arena, 1860-1920. University of California Press. ku. 199–. ISBN 978-0-520-24946-2. Iliwekwa mnamo 29 Julai 2012.
  2. Amarjit, Chandan (S p r i n g 2 0 0 7). "Punjabis in East Africa" (PDF). I A S N e w s l e t t e r. Iliwekwa mnamo 29 Julai 2012. {{cite web}}: Check date values in: |year= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  3. "The Standard (Kenyan newspaper) -- Britannica Online Encyclopedia". britannica.com. 2012. Iliwekwa mnamo 29 Julai 2012.
  4. Zarina Patel (2002). Alibhai Mulla Jeevanjee. East African Publishers. ISBN 978-9966-25-111-4. Iliwekwa mnamo 29 Julai 2012.
  5. Patel, Zarina (31 Oktoba 2011). "The Struggle to Preserve Jeevanjee Gardens". awaazmagazine.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 29 Julai 2012.