Nenda kwa yaliyomo

Alessandro Volta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Alessandro Volta
Seli ya Galvani iliboreshwa na Volta aliyeunganisha seli kadhaa kuunda beteri ya kwanza

Alessandro Giuseppe Antonio Anastasio Volta (matamshi ya Kiitalia: [alessandro vɔlta]; 18 Februari 1745 - 5 Machi 1827) alikuwa mwanafizikia wa Italia, aliyegundua kanuni za misingi za umeme. Aliboresha seli ya Luigi Galvani akatengeneza betri ya kwanza kwa kuunganisha seli kadhaa mwaka 1799.

Kwa uvumbuzi huo Volta ameonyesha kwamba umeme unaweza kuzalishwa kikemia. Uvumbuzi wa Volta ulisababisha msisimko mkubwa wa kisayansi na kuongoza wengine kufanya majaribio kama hayo ambayo hatimaye yalileta maendeleo ya uwanja wa kemia ya umeme.

Alessandro Volta pia alimvutia Napoleon Bonaparte katika uvumbuzi wake, na alialikwa kwenye Taasisi ya Ufaransa ili kuonyesha uvumbuzi wake kwa wanachama wa Taasisi hiyo. Alessandro Volta alikuwa profesa wa fizikia ya majaribio katika Chuo Kikuu cha Pavia kwa karibu miaka 40 na alipendwa sana na wanafunzi wake.

Licha ya mafanikio yake ya kitaaluma, Volta alitamani kuwa mtu anayeelekea katika maisha ya ndani na hii ilikuwa inaonekana zaidi katika miaka yake ya baadaye. Wakati huu yeye alitamani kuishi salama na maisha ya umma na zaidi kwa ajili ya familia yake mpaka hatimaye alikufa mwaka 1827.


Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alessandro Volta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.