Nenda kwa yaliyomo

Airbus A300

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
A300.

Airbus A300 ni ndege inayotumia injini pacha na imezalishwa na Airbus.

Ilitangazwa rasmi mwaka 1969 na kuanza kuruka mnamo Oktoba 1972, Pia ilikuwa bidhaa ya kwanza ya Airbus Industrie, muungano wa wazalishaji wa ndege Ulaya, sasa ni kampuni ndogo ya Airbus. A300 kwa kawaida inaweza kupakia abiria 266 na kuruka maelfu ya kilomita.

Maendeleo ya A300 ilianza wakati wa miaka ya 1960 kama mradi wa Ulaya kati ya wazalishaji mbalimbali wa ndege nchini Uingereza, Ufaransa na Ujerumani Magharibi.

Mnamo Septemba 1967, mataifa yaliyoshiriki yalitia saini Mkataba wa kutengeneza ndege. Waingereza walijitoa kwenye mradi huo tarehe 10 Aprili 1969. Mkataba mpya ulifikiwa kati ya Ujerumani na Ufaransa tarehe 29 Mei 1969, na Airbus Industrie iliundwa rasmi tarehe 18 Desemba 1970 ili kuendeleza na kuzalisha A300. Aina ya kwanza iliondoka tarehe 28 Oktoba 1972.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.