Agatha Christie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jalada lenye picha ya Agatha Christie.

Agatha Mary Clarissa Christie (15 Septemba 1890 - 12 Januari 1976) alikuwa mwandishi wa riwaya za jinai kutoka nchini Uingereza. Vitabu vyake ni maarufu sana ulimwenguni kote, na zaidi ya nakala bilioni 4 ziliuzwa ulimwenguni. Vitabu vyake vimetafsiriwa kwa lugha 103 tofauti.

Riwaya zake ni juu ya mauaji na ugunduzi wake. Kwa kawaida ugunduzi ni kazi tata. Katika masimulizi yake kuna mpelelezi ambaye anajaribu kumkamata mwuaji akifauli mwishowe.

Wahusika wanaorudia kupatikana katika hadithi ni Miss Marple na Hercule Poirot . Miss Marple ni mama mzee Mwiingereza anayezungumza na kila mtu. Watu hawadhani yeye ni mwerevu, lakini kila wakati yeye hutambua mtu mbaya ni nai. Hutumia mantiki kujua nani ana hatia ya mauaji.

Hercule Poirot ni mtu wa ajabu, mpelelezi wa kibinafsi kutoka Ubelgiji anayeishi London . Anapenda kujua ni nani aliyefanya mauaji kwa kufikiria juu ya ushahidi wote. Hadithi za Poirot na Miss Marple zilifanywa kuwa vipindi vingi vya Runinga na filamu za sinema.

Christie pia aliandika tamthiliya. Moja inayoitwa The Mousetrap (Mtego wa Panya) ilianza kuonyeshwa zaidi ya miaka 60 iliyopita ikiwa ni tamthiliya ineyoendelea kwa muda mrefu duniani.

Christie alizaliwa Torquay huko Devon, Uingereza. Yeye hakuenda shule. Alikupata masomo nyumbani akifundishwa na mamake aliyeamini watoto hasianze kusoma hadi wawe na umri wa miaka nane. Lakini Christie alijifundisha kusoma mwenyewe wakati alikuwa na miaka minne. Alisoma vitabu vingi na hivyo alijifunza kuwa mwandishi mzuri. Aliendelea kuwa mpiga piano mzuri na mwimbaji, pia. Alikuwa ameolewa mara mbili; alimzaa binti mmoja aliyeitwa Rosalind Hicks.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alijitolea kufanya kazi katika hospitali na katika duka la dawa.

Mnamo 1971, aliheshimiwa na Malkia kwa kupewa cheo cha Kamanda wa Kike wa Order of the British Empire.

Christie aliaga dunia tarehe 12 Januari 1976 akiwa na umri wa miaka 85 katika nyumba yake ya Winterbrook kwenye parokia ya Cholsey huko Oxfordshire (zamani sehemu ya Berkshire). Amezikwa katika makaburi ya kanisa la St Mary's, Cholsey .

Kitabu cha Rekodi za Dunia za Guiness kinamtaja Christie kama mwandishi wa riwaya zilizouzwa kushinda riwaya za mwandishi mwingine yeyote. Riwaya zake zimeuza karibu nakala bilioni 4. Vitabu vilichapishwa zaidi baada ya vile vya William Shakespeare na Bibilia . Vitabu vyake vimetafsiriwa kwa angalau lugha 103. Riwaya inayouzwa zaidi kwa Christie ni And then there were none iliyotolewa mara milioni 100. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Davies, Helen (14 Septemba 2007). "21 Best-Selling Books of All Time". Editors of Publications International. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Aprili 2010. Iliwekwa mnamo 2009-03-25.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)