Nenda kwa yaliyomo

Abacavir/lamivudine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Combination of
Abacavir Analogi ya nucleotiidi kizuizi cha nakala rudufu ya nyuma
Lamivudine Analogi ya nucleotiidi kizuizi cha nakala rudufu ya nyuma
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Kivexa, Epzicom, mengineyo
MedlinePlus a696011
Kategoria ya ujauzito C(US)
Hali ya kisheria Prescription Only (S4) (AU) POM (UK) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
 N(hii ni nini?)  (thibitisha)

Abacavir/lamivudine, inayouzwa chini ya jina la chapa Kivexa miongoni mwa mengineyo, ni dawa mchanganyiko ya dozi isiyobadilika inayotumika kutibu VVU/UKIMWI. [1] Ina abacavir na lamivudine.[1] Inapendekezwa kwa ujumla kwa matumizi na dawa zingine za kurefusha maisha.[1] Mara nyingi hutumiwa kama sehemu ya tiba inayopendekezwa kwa watoto.[2] Inachukuliwa kwa mdomo kama tembe. [1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na shida ya kulala, maumivu ya kichwa, unyogovu, hisia ya uchovu, kichefuchefu, upele na homa.[1] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha viwango vya juu vya lactate katika damu, athari ya mzio na kuongezeka kwa ukubwa wa ini.[1] Haipendekezwi kwa watu walio na jeni maalumu inayojulikana kama HLA-B*5701.[1] Usalama wa mayumizi yake katika ujauzito haujasomwa vizuri lakini inaonekana kuwa sawa.[3] Lamivudine na abacavir zote ni vizuizi vya nucleoside reverse transcriptase (NRTI).[1]

Abacavir/lamivudine iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2004.[1] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[4] Gharama ya jumla katika nchi zinazoendelea ilikuwa takriban dola 14.19 hadi 16.74 kwa mwezi kufikia mwaka wa 2014.[5] As of 2015, gharama ya mwezi wa kawaida wa dawa nchini Marekani ni zaidi ya dola 200.[6]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 "Abacavir and Lamivudine Tablets". Teva Pharmaceuticals USA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Februari 2017. Iliwekwa mnamo 28 Novemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. World Health Organization (2015). The selection and use of essential medicines. Twentieth report of the WHO Expert Committee 2015 (including 19th WHO Model List of Essential Medicines and 5th WHO Model List of Essential Medicines for Children). Geneva: World Health Organization. ku. 45–46. hdl:10665/189763. ISBN 9789241209946. ISSN 0512-3054. WHO technical report series;994.
  3. "Abacavir / lamivudine (Epzicom) Use During Pregnancy". www.drugs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Desemba 2016. Iliwekwa mnamo 4 Desemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
  5. "Abacavir + Lamivudine". International Drug Price Indicator Guide. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Januari 2018. Iliwekwa mnamo 28 Novemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Hamilton, Richart (2015). Tarascon Pocket Pharmacopoeia 2015 Deluxe Lab-Coat Edition. Jones & Bartlett Learning. uk. 59. ISBN 9781284057560.