Yosafat wa Polotsk
Yosafat wa Polotsk (1580 hivi – 1623) alikuwa askofu wa Polotsk (leo nchini Belarus).
Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake ni tarehe 12 Novemba[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Yosafat Kuntsevych (kwa Kibelarus Язафат Кунцэвіч, Jazafat Kuncevič) alizaliwa Wlodzimierz Wolynski katika mkoa wa Volinia (ulikuwa sehemu ya Lithuania, leo ni ya Ukraina) mwaka 1580 au 1584 katika familia ya Waorthodoksi akaitwa Yohane katika ubatizo.
Baada ya kusoma Vilnius (Lithuania), mwaka 1604 alijiunga na Wakatoliki wa mashariki waliokubali mapatano ya Muungano wa Brest yaliyoanzisha Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina. Akajiunga na wamonaki wa mtakatifu Basili Mkuu kwa jina la kitawa Yosafat.
Alipata upadri, akateuliwa kuwa askofu wa Polotsk. Alijitahidi kutunza kwa makini liturujia ya Kiorthodoksi na kuhimiza wote kwa ari ya kudumu kwenye umoja na Kanisa Katoliki kwa jumla.
Alifanya kazi kubwa sana kutunza urithi huo wa pekee wa Kanisa lake hadi mwaka 1623 alipouawa na umati wa Waorthodoksi waliopinga umoja huo, akifa kwa ajili ya Kanisa Katoliki na ukweli wake[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Maisha yake kwa Kiingereza katika Catholic Forum Ilihifadhiwa 29 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- St. Josaphat Kuncevyc katika Catholic Encyclopedia
- Patron Saints Index: Saint Josaphat Ilihifadhiwa 10 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |