Wikipedia:Makala ya wiki/Leonardo da Vinci

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Leonardo da Vinci

Leonardo da Vinci (15 Aprili 14522 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipaji vingivingi kutoka nchini Italia. Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifu majengo, mwanabotania, mwanamuziki, na mwandishi.

Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika masomo, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa muda wote. Watu wengi hufikiria kwamba alikuwa mtu aliyebarikiwa vipaji katika historia ya maisha.

Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema kwamba hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake unaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti". Leonardo alizaliwa Vinci, mji mdogo ulio karibu na Firenze nchini Italia. Alifunzwa kuwa msanii na mchongaji na mchoraji Verrocchio.

Alitumia sehemu kubwa ya maisha yake akimtumikia tajiri mmoja maarufu wa Kiitalia. Katika miaka yake ya mwisho aliishi katika nyumba yake nzuri aliyopewa na Mfalme wa Ufaransa. Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Miongoni mwa picha zake mbili maarufu duniani ni pamoja na Mona Lisa na Karamu ya Mwisho. Amefanya michoro mingi sana. Mchoro mmojawapo unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro. ►Soma zaidi