Wikipedia:Makala ya wiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maelezo
Ukitaka kupeleka makala hapa (itaonekana baadaye kwenye ukurasa wa Mwanzo kwa kubadilishana na nyingine)

  1. A) Chagua makala unaotaka kuonyesha kwenye ukurasa wa kwanza
  2. B) tunga hitimisho fupi ya makala hii (si zaidi ya alama 1100) na kuihifadhi kwa jina la Wikipedia:Makala ya wiki/XXXXXXX - badala ya XXXXXXX andika jina la makala
  3. Andika jina la makala uliyotunga hapa badala ya jina la nyingine. Usiongeze idadi kwa jumla!
  4. katika makala hii kopi Kigezo:Makala ya wiki
|jina= (jina la makala) Badala ya mabano andika jina la makala.
|picha= (jina la picha) Badala ya mabano andika jina la faili ya picha.
|nakala ya picha = (matini itakayoonekana chini ya picha) Badala ya mabano andika maelezo ya picha.
|makala = (sehemu ya makala uliyochagua - izizidi alama 1100 - 1150) Badala ya mabano andika sehemu ya makala uliyochagua - izizidi alama 1100. Tofauti na kawaida weka maneno ya kwanza yenye jina la makala kwa mabano mraba mfano [[Wolfgang Amadeus Mozart]] maanake hii inasidia kufungua makala yenyewe.

Mwisho wa maelezo - hariri chini yake


(maelezo ya picha)

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) (ing. Tanzania People's Defense Force TPDF) ni jeshi lililoanzishwa mnamo mwezi wa Septemba katika mwaka wa 1964. Ilichukua nafasi ya jeshi la Tanganyika Rifles lililorithiwa na ukoloni wa Kiingereza. Chanzo cha jeshi nchini Tanzania kilikuwa jeshi la kikoloni la Uingereza katika Afrika ya Mashariki. Mwaka 1919 Uingereza ilikabidhiwa utawala juu ya Tanganyika na Shirikisho la Mataifa. Baada ya uhuru mwaka 1961 vikosi vya King's African Rifles katika Tanganyika vilibadilishwa jina na kuwa Tangayika Rifles (TR). Pamoja na kubadilika jina Tanganyika Rifles ilikuwa na muundo sawa na Kings African Rifles (KAR). Maafisa wenye mamlaka bado walikuwa Waingereza, pamoja na Waafrika watano waliopandishwa cheo wakati wa uhuru na kupokea mafunzo katika vyuo vya kijeshi vya Kiingereza. Jeshi jipya lilipangwa katika vikosi viwili vyenye makao makuu huko Dar es Salaam na Tabora. Afisa mkuu alikuwa Brigedia Jenerali Patrick Sholto Douglas. Kwa jumla kulikuwa na hali ya kutoridhika kati ya askari wa TR. Sababu yake ilikuwa matumaini ya kwamba uhuru ungeleta mabadiliko makubwa zaidi na nafasi za kupanda cheo baada ya kuondoka kwa maafisa wazungu. Lakini maafisa Waingereza waliendelea kuajiriwa na serikali ya Nyerere na tofauti kubwa katika mapato na hali ya makazi ya Wazungu na Waafrika ziliendelea. ►Soma zaidi