Umeme wa upepo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
UWezo wa miradi ya umeme wa upepo iliyoanzishwa duniani kati ya 1996 na 2008
Mradi wa Umeme wa Upepo Fenton Wind Farm katika Minnesota (Marekani).

Umeme wa upepo ni umeme unaopatikana kwa njia ya mitambo inayotumia nguvu ya upepo na kuibadilisha kuwa umeme. [1]

Mwisho wa mwaka 2009 takriban asilimia 1.3 ya mahitaji ya umeme duniani zilikuwa umeme wa upepo. [2] Lakini nchi kadhaa zilizotangulia kuendesha teknolojia hii zinapata kiasi kikubwa zaidi. Nchi inayopata kiwango kikubwa cha mahitaji yake ya umeme ni Denmark yenye asilimia 20 za umeme wa upepo. [3][4] Katika Hispania ni 11% na 9% katika Eire. [5]

Katika Afrika ni hasa Afrika Kusini iliyoanza kutumia chanzo hiki cha nishati. Nchini Kenya Mradi wa umeme wa upepo wa Ziwa Turkana ulianzishwa mwaka 2010 unaotegea kutoa megawati 300 baada ya kukamilika.[6]

Jinsi ya kutumia nguvu ya upepo [hariri]

Upepo hutumiwa kuzungusha rafadha au parapela. Mwendo wa rafadha inaendelea kuzungusha jenereta ya kutoa umeme.

Marejeo ya Nje [hariri]