Nenda kwa yaliyomo

The Lion King

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The Lion King

Posta ya filamu hii iliyochorwa na John Alvin[1]
Imeongozwa na Roger Allers
Rob Minkoff
Imetayarishwa na Don Hahn
Imetungwa na Irene Mecchi
Jonathan Roberts
Linda Woolverton
Nyota Matthew Broderick
Jeremy Irons
James Earl Jones
Jonathan Taylor Thomas
Nathan Lane
Ernie Sabella
Moira Kelly
Robert Guillaume
Rowan Atkinson
Whoopi Goldberg
Cheech Marin
Jim Cummings
Muziki na Songs:
Elton John
Tim Rice
Lebo M
Score:
Hans Zimmer
Imehaririwa na Ivan Bilancio
Imesambazwa na Walt Disney Pictures
Imetolewa tar. 15 Juni 1994 (miji iliyochaguliwa)
24 Juni 1994 (kwa ujumla)
18 Novemba 1994 (kutolewa upya)
25 Desemba 2002 (IMAX kutolewa upya kwa toleo maalum)
Ina muda wa dk. 90
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu $45,000,000
Mapato yote ya filamu $783,841,776
Ikafuatiwa na The Lion King II: Simba's Pride

The Lion King (Kiswahili: Mfalme Simba) ni filamu ya katuni iliyotolewa mwaka wa 1994. Filamu ilitayarishwa na Walt Disney Feature Animation, na kutolewa kwenye makumbi mnamo tar. 15 Juni 1994 na Walt Disney Pictures. Hii ni ya 32 kutolewa kwa mujibu wa orodha ya filamu za katuni za Walt Disney. Hadithi hii, ilifananishwa kabisa na ile hadithi ya mchezo wa William Shakespeare wa Hamlet. Hadithi hii imechezwa kama ikiwa inaeleza ufalme wa wanyama wa Afrika.[2] Filamu imepata kuwa moja kati ya filamu zenye mapato makubwa ya karne hadi hapo ilipokuja kutolewa filamu nyingine ya katuni ya Finding Nemo (Disney/Pixar). The Lion King bado inashikiria taji lake la kuwa filamu yenye mapato makubwa katika historia ya makundi ya filamu za kiasili (wanyama)[3] na inamilikiwa katika kipindi kijulikanacho cha Mwamko wa Disney.[4]

Simba ni mtoto wa kiume wa Mufasa, na Mufasa ndiyo simba mfalme anayemiliki sasa ufalme uitwao Pride Rock. Lakini, ndugu mdogo wa Mufasa (Scar) anamwonea choyo Simba na Mufasa wanataka kumweka Mufasa kuwa kama mfalme wa falme hiyo. Scar hawezi kuwa mfalme isipokuwa akifa Mufasa na Simba. Scar akawa rafiki na fisi watatu na kuwaahidi kwamba atawapatia chakula endapo watamsaidia kumwua ndugu yake Mufasa na Simba na kuchukua mamlaka ya ufalme huo.

Scar na wale mafisi wakamtega Simba kule pembezoni mwa mto, mahali ambapo Scar akatuma midudu mikubwa ya mwituni iende kumwua. Mufasa akashitukia mpango huo kwamba mtoto wake yupo hatarini hivyo akaenda mbio kumwokoa. Akaruka chini kule kwenye eneo la fujo na kumvuta Simba nje kabla hajauawa na kumtupia juu ya jiwe ambapo atakuwa yupo salama. Hata hivyo, pale Mufasa alipokuwa akijaribu kupalamia jabali ili awe salama, Scar akaja kwa juu yake na kumsukumia chini ya lile jebali.

Hivyo Mufasa akaangukia ndani ya lile eneo la fujo na kufa. Scar bado akawa anajifanya anataka kupatana na Simba kabla Scar hajawa mfalme, na kujifanya kumweleza Simba kwamba kule kufa kwa Mufasa ni kosa lake. Hivyo ataondoka na asirudi tena. Halafu baadaye akaenda kuwaambia wale jamaa zake wa awali (fisi) waende kumwua Simba.

Wakawa wanamtoa mbio Simba hadi kule chini ya mipungate, lakini bado Simba alitoweka. Mmoja kati ya wale fisi akajibwenga katika ile mipungate na kupiga kelele kuubwa. Simba bado akawa anamkimbia yule fisi mmoja (aitwaye Banzi) akawa anawaambia wenziwe waendelee kumkimbiza Simba, lakini Sheinzi, fisi wa pili (wa tatu wake ni bwege anaitwa Ed) akasema "Hakuna jinsi mimi ninakwenda kule! Unasemaje, unataka na mimi nije kuwa kama wewe, Popo-Mpungate?!" Kwa hiyo wakamwachia Simba aende zake, huku wakiwa wanapiga zogo wakiwa kwa juu.

Muda huohuo, Scar akaanza kumwambia kila mtu kuhusu ile vulumai, na akasema kwamba Simba tu ndiye aliyekufa, bila kujua ukweli kwamba wakina fisi hawajaweza kumwua Simba. Halafu akachukua ufalme na kuwa mfalme wa hapa, tangu hapo akawa mtu karibu sana katika familia. Simba alikua huku akiwa na marafiki zake wapya wawili, Timon na Pumbaa. Amejifunza kuishi na wito mpya, "Hakuna matata", ambayo kwa kuilezea zaidi inamaana ya "Hamna Shida".

Simba alikua huku akiwa shupavu kwelikweli pale alipojiunga na rafiki yake wa udogoni Nala, ambaye alikuwa akijua kwamba baba yake Mufasa yu hai. Alimweleza kuhusu mambo ya kishenzi anayoyafanya Scar na kumwomba Simba arudi ili apambane na Scar. Simba akarudi zake nyumbani na kuanza kupambana na Scar kwa ajili ya ufalme, na ikatokea Scar akaeleza ukweli kwamba yeye ndiye aliyemwua Mufasa. Kulikuwa mapigano ya muda mrefu, lakini Simba akamshinda Scar, akadai kwamba yeye ana haki ya kuwa mfalme. Nala akawa malkia wa Simba na wakazaa kitoto chao wenyewe.

Washiriki

[hariri | hariri chanzo]
  1. Stewart, Jocelyn. "Artist created many famous film posters", Los Angeles Times, 2008-02-10. Retrieved on 2008-02-10. 
  2. The Lion King: Platinum Edition (Disc 2), Origins. [DVD]. Walt Disney Home Entertainment.
  3. "Highest grossing animated films", Box Office Mojo. Retrieved on 2008-07-29. 
  4. "Disney: Notes on the end of the Disney Renaissance". decentfilms.com. Iliwekwa mnamo 2008-08-26.

Viuongo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: