Sixtus Raphael Mapunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sixtus Raphael Mapunda ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Mbinga Mjini kwa miaka 20152020.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa tarehe 13 Agosti 1979 katika Hospitali ya Litembo iliyopo Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma.

Alisoma mwaka 1987 mpaka 1993 katika shule ya msingi Litembo.

Mwaka 1994 alijiunga na seminari ndogo ya Liganga Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.

Mwaka 1995 alijiunga na Seminari ya Likonde, ambapo alisoma mpaka kidato cha tatu na baadae mwaka 1998 akahamia Sekondari ya Meta Mkoani Mbeya ambapo alimaliza kidato cha nne. Mwaka 1999 alichaguliwa kujiunga Kigonsera High School, hata hivyo hakuenda kuripoti kutokana na mashauriano na rafiki yake wa karibu.

Alimaliza kidato cha sita mwaka 2001 akajiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 mpaka 2005. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017