Scott Storch

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Scott Storch
Jina la kuzaliwa Scott Storch
Amezaliwa 16 Desemba 1973 (1973-12-16) (umri 50)
Asili yake Nova Scotia, Kanada
Aina ya muziki Hip hop, R&B , reggaeton
Kazi yake Mtayarishaji, rapa
Ala Kinanda, sampler ngoma,
Miaka ya kazi 1993 – hadi leo
Studio SMC, InterscopeTuff Jew Produtions
Tovuti Scott Storch katika MySpace

Scott Storch (amezaliwa tar. 16 Desemba 1973) ni mtayarishaji wa rekodi za muziki kutoka nchini Kanada.[1][2] Amejipatia mafanikio kedekede kwenye medani ya muziki mbalimbali, hasa katika hip hop, pop, na R&B. Ana studio yake iitwayo Storch Music Company na pia anamiliki kampuni ya muziki iitwayo Tuff Jew Productions LLC.

Storch, amepata kutayairisha kazi za wasanii kibao. Wasanii hao ni pamoja na Dr. Dre, Ice Cube, Tag Team Music, Fat Joe, Ja Rule, Mariah Carey, Toni Braxton, Raven Symone, Jadakiss, Daddy Yankee, Eminem, Christina Aguilera, Nas, T.I., Lil Wayne, Nelly, Paris Hilton, Jessica Simpson, 50 Cent, Beyoncé, Brooke Hogan, LeToya Luckett, Danity Kane, The Game, Tha Realest, Chamillionaire, Ras Kass, Chingo Bling, Kelly Rowland, Teairra Mari, Chris Brown, na wengine kibao. Kwa sasa ana fanya kazi na msanii wa R&B - Ciara katika albamu yake mpya itakayo toka ("Fantasy Ride") mwanzoni mwa mwaka wa 2009.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali na muziki[hariri | hariri chanzo]

Scott alizaliwa mnamo 1973 mjini Nova Scotia, Kanada. Storch ni mtoto wa Mzee Fahad, ambaye ni mwendesha mashtaka na mwimbaji, ambao wote wanaasili ya Kiyahudi. Kwa bahati baadaye alihamia mjini Cherry Hill Township, New Jersey halafu Coral Springs, Florida.

Alijiunga na shule ya Davie, Florida, lakini baadaye aliachana na shule hiyo na kuamua kujiendeleza na masuala ya muziki. Akiwa na umri wa miaka 16, akaja kuwa mpiga kinanda wa bendi ya muziki wa rap na hip hop maarufu kama The Roots. Rekodi za bendi hiyo, zikawa za juu zaidi na kuweza kuapata mafanikio kibao. Lakini baadaye Scott aliachana na bendi kwa sababu ana sema kwamba "ina hitajika hatua za awali zipelekwe mbele zaidi".

Kibao cha kwanza cha Storch kuwika, pale alikutana na Dr. Dre, na kujaribu kumsaidia kutayarisha wimbo wa "Still D.R.E." Pia ana shauku na mtindo wa muziki wa Mashariki ya Kati na muziki wa Kihndi pia, na ndiyo maana amekuha kuutumia mtindo huo katika baadhi ya nyimbo hizi, "Lean Back" ya Fat Joe, "Candy Shop" na "Just a Lil' Bit" ya 50 Cent, "Side Effects" ya Mariah Carey, "Turn It Up" ya Paris Hilton, "Poppin' Them Thangs" ya G-Unit, "Let Me Love You" ya Mario, "Playa's Only" ya R. Kelly (akimshirkisha The Game), "Lock U Down" ya Mýa, na vilevile "Naughty Girl" na "Baby Boy", zote mbili za Beyoncé, "About Us" ya Brooke Hogan, na "Turn It Up" ya Chamillionaire, na "Work" ya Kelly Rowland.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. e-Talk Daily, December 6, 2006. CTV (2006-11-06). Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-04-19. Iliwekwa mnamo 2007-01-25.
  2. Breaking News: Scott Storch Missing, July 24, 2008. RRT (2008-07-24). Iliwekwa mnamo 2008-07-25.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]