Dr. Dre

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dr. Dre
Dr. Dre mnamo 2011
Dr. Dre mnamo 2011
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Andre Romelle Young
Amezaliwa 18 Februari 1965 (1965-02-18) (umri 59)
Asili yake Los Angeles, California, Marekani
Aina ya muziki Hip hop, West Coast hip hop, Electronic rap, Gangsta funk, Gangsta rap
Kazi yake Rapa, mtayarishaji wa rekodi
Ala Sauti, synthesizer, Kinanda, fonografia, mashine ya ngoma
Miaka ya kazi 1984–hadi leo
Studio Epic, Ruthless, Priority, Death Row, Aftermath, Interscope
Ame/Wameshirikiana na Eazy E, Ice Cube, The D.O.C, Snoop Dogg, N.W.A, 2Pac, Eminem, 50 Cent, The Game, Shade Sheist, Busta Rhymes, Xzibit, Royce Da 5'9", Jay-Z, Nas, Blackstreet, Stat Quo, Bishop Lamont, MC Ren, Obie Trice
Tovuti Dre2001.com

Andre Romelle Young (alizaliwa tar. 18 Februari 1965) ni mtayarishaji wa rekodi, rapa, na mmiliki wa studio ya rekodi za muizki kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Dr. Dre. Dre ni mwanzilishi na mmiliki wa sasa Aftermath Entertainment na mmiliki mshiriki-msanii wa zamani wa studio ya Death Row Records, na pia kutayarisha albamu kadhaa kwa ajili yake na wasanii wengine kadhaa wa rekodi hiyo kama vile Snoop Dogg na Eminem.

Akiwa kama mtayarishaji, amejipatia sifa sana kwa kuukuza muziki wa West Coast G-funk, staili ya muziki wa rap unaotengenezwa na synthesizer-yenye ya taratibu, na mdundo wa nguvu.

Dr. Dre alianza shughuli za muiki akiwa kama mmoja kati ya wanamchama wa kundi la muziki la World Class Wreckin' Cru na kisha baadaye akaanzisha kundi lenye athira kubwa ya gangsta rap la N.W.A, ambayo ilivuma sana kwa mashairi yake mazito yenye kutaja maisha ya kiharifu na mtaani kwa ujumla.[1] Mnamo mwaka wa 1992, alitoa albamu kama msanii wa kujitegemea. Na albamu ilikwenda kwa jina la The Chronic, ilitolewa ikiwa chini ya Death Row Records, na kumpelekea kuwa mmoja katia ya wasanii waliouza rekodi bora za muziki wa Marekani kwa mwaka wa 1993[2] na kushinda Tuzo ya Grammy kwa ajili ya single ya "Let Me Ride".

Mnamo mwaka wa 1996, aliondoka Death Row na kwenda kuanzisha studio yake mwenyewe ya Aftermath Entertainment, na kutoa albamu ya mchanganyiko ya Dr. Dre Presents the Aftermath, kunako 1996, na ksiha baadaye akatoa albamu yake nyingine iliyokwendwa kwa jina la 2001, kunako 1999, ambayo ili mfanya ashinde Tuzo ya Grammy akiwa kama mtayarisha bora.

Kunako miaka ya 2000, aliekeza shughuli zake za utayarishaji wa muziki kwa wasanii wengine, wakati muda huo akawa anashiriki katika kutia sauti kwenye baadhi ya nyimbo za wasanii wengine.

Rolling Stone wamemwita ni mmoja kati ya wasanii waliolipwa pesa nyingi sana kwa mwaka wa 2001[3] na 2004.[4] Dr. Dre also had acting roles in the 2001 films The Wash and Training Day.[5]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa akiwa kama mtoto wa kwanza wa Verna na Theodore Young, Dr. Dre alizaliwa na jina la André Romelle Young mnamo tar. 18 Februari 1965, wakati mama yake akiwa na umri wa miaka 16. Ameolewa na baba yake, Theodore Young, baada ya kuzaliwa kwake. Jina lake la kati, "Romelle," linatoka katika jina la Theodore Young, ambalo ni jina la kundi la kuimba muziki wa R&B wa lidhaa, The Romells. Mnamo mwaka wa 1968 mama yake akatarikiwa na Theodore Young na kisha baadaye akaja kuoelewa na Curtis Crayon. Kwa pamoja wakaja kuzaa tena mitoto mitatu, wawili wa kiume Jerome na Tyree (wote wamefariki) na binti mmoja aliyeitwa Shameka.

Mnamo mwaka wa 1976 Young akapata kujiunga na shule ya Vanguard Junior High School, lakini kwa kufuatia vurugu, fujo na uhuni uliojaa katika shule ya Vanguard, akahamishwa katika kitongoji kilichosalama kabisa katika shule ya Roosevelt Junior High School.[6] Baadaye Verna akajakuolewa na Warren Griffin, ambaye alikutana naye katika eneo la kazi yake mpya huko Long Beach,[7] ambaye yeye ndiye aliongeza madada wengine watu na mkaka mmoja katika familia. Huyo ndugu wa kiume, Warren Griffin III, ambaye baadaye alikuja kuwa na rapa na kujiita Warren G.[8]

Young alielekeza zake tena katika shule ya Centennial High School ya mjini Compton wakati wa ujana wake mnamo mwaka wa 1979, lakini alihamisha katika shule ya Fremont High School kwa kufuatia viwango vidogo. Young akathubutu kujiandikisha katika kampuni moja iitwayo Northrop Aviation Company kwa mpango wa kujiendeleza kivitendo, lakini viwango vidogo vya shuleni vimefanya awe hafai. Baada ya hapo, akaamua kulenga maisha yake ya kijamii katika masuala ya burudani kwa ajili ya maisha yake ya shule.[9] Young akapata mtoto wa kiume, Curtis, aliyezaliwa tar. 15 Desemba 1981, na Lisa Johnson. Curtis Young alilelewa na mama yake na hajaonana na baba yake hadi Curtis alipokuja kuwa rapa akiwa na umri wa miaka 20 hapo baadaye, akiwa na jina la kisanii la Hood Surgeon.[10]

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Albamu[hariri | hariri chanzo]

Albamu za studio[hariri | hariri chanzo]

Albamu za filamu[hariri | hariri chanzo]

Albamu za ushirikiano[hariri | hariri chanzo]

akishirikiana na World Class Wreckin' Cru

akishirikiana na N.W.A.

Tuzo na mapendekezo[hariri | hariri chanzo]

Tuzo za Grammy[hariri | hariri chanzo]

Dr. Dre ameshinda Tuzo za Grammy mara sita. Tatu kati ya hizo ni kwa kazi yake ya utayarishaji.[11][12][13]

Mwaka Kazi iliyoteuliwa Tuzo Matokeo
1990 "We're All in the Same Gang" Best Rap Performance by a Duo or Group Nominated
1994 "Nuthin' but a 'G' Thang" (with Snoop Doggy Dogg) Nominated
"Let Me Ride" Best Rap Solo Performance Ameshinda
1996 "Keep Their Heads Ringin'" Nominated
1997 "California Love" (with 2Pac & Roger Troutman) Best Rap Performance by a Duo or Group Nominated
1998 "No Diggity" (with Blackstreet & Queen Pen) Best R&B Song Nominated
2000 "Still D.R.E." (with Snoop Dogg) Best Rap Performance by a Duo or Group Nominated
"Guilty Conscience" (with Eminem) Nominated
2001 "Forgot About Dre" (with Eminem) Ameshinda
"The Next Episode" (with Snoop Dogg, Kurupt & Nate Dogg) Nominated
The Marshall Mathers LP (as engineer) Album of the Year Nominated
Best Rap Album Ameshinda
2001 Nominated
Himself Producer of the Year, Non-Classical Ameshinda
2002 Nominated
2003 Nominated
"Knoc" (with Knoc-turn'al & Missy Elliott) Best Music Video, Short Form Nominated
The Eminem Show (as producer) Album of the Year Nominated
2004 "In da Club" (as songwriter) Best Rap Song Nominated
2006 Love. Angel. Music. Baby. (as producer) Album of the Year Nominated
"Encore" (with Eminem & 50 Cent) Best Rap Performance by a Duo or Group Nominated
2010 "Crack a Bottle" (with Eminem & 50 Cent) Ameshinda
Relapse (as engineer) Best Rap Album Ameshinda
2011 Recovery (as producer) Album of the Year Nominated
2012 "I Need a Doctor" (with Eminem & Skylar Grey) Best Rap/Sung Collaboration Nominated
Best Rap Song Nominated
2014 good kid, m.A.A.d city (as featured artist) Album of the Year Nominated
2016 Compton Best Rap Album Nominated
2017 Straight Outta Compton Best Compilation Soundtrack for Visual Media Nominated

MTV Video Music Awards[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Kazi iliyopendekezwa Tuzo Matokeo
1993 "Nuthin' But a "G" Thang" Best Rap Video Nominated
1994 "Let Me Ride" Nominated
1995 "Keep Their Heads Ringin'" Ameshinda
1997 "Been There, Done That" Nominated
Best Choreography in a Video Nominated
1999 "My Name Is" Best Direction Nominated
"Guilty Conscience" Breakthrough Video Nominated
2000 "The Real Slim Shady" Best Direction in a Video Nominated
2000 "Forgot About Dre" Best Rap Video Ameshinda
2001 "Stan" Best Direction in a Video Nominated
2009 "Nuthin' But a "G" Thang" Best Video (That Should Have Won a Moonman) Nominated

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Films
Mwaka Jina Nafasi Maelezo
1992 Niggaz4Life: The Only Home Video Himself Documentary
1996 Set It Off Black Sam Minor Role
1999 Whiteboyz Don Flip Crew #1 Minor Role
2000 Up In Smoke Tour Himself Concert Film
2001 Training Day Paul Minor Role
2001 The Wash Sean Main Role
2015 Unity[14] Narrator Documentary
2017 The Defiant Ones[15] Himself Documentary
Michezo ya video
Mwaka Jina Nafasi Maelezo
2005 50 Cent: Bulletproof Grizz Voice role and likeness
Filamu za wasifu
Mwaka Jina Mwigizaji Maelezo
2015 Straight Outta Compton Corey Hawkins Biographical film about N.W.A
2016 Surviving Compton: Dre, Suge & Michel'le Chris Hamilton Biographical film about Michel'le
2017 DPG 4 Life: Tha Movie Curtis Young[16] Biographical film about Tha Dogg Pound
All Eyez on Me Harold Moore[17] Biographical film about Tupac Shakur


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Erlewine, Stephen Thomas (2000). Dr. Dre - Biography. Allmusic. Iliwekwa mnamo 2007-09-22.
  2. Holden, Stephen. "The Pop Life", The New York Times, 1994-01-14. Retrieved on 2008-03-03. 
  3. LaFranco, Robert; Binelli, Mark; Goodman, Fred (2002-06-13). U2, Dre Highest Earning Artists. Rolling Stone. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-02-22. Iliwekwa mnamo 2006-12-08.
  4. LaFranco, Robert (2005-02-10). Money Makers. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-04-02. Iliwekwa mnamo 2006-12-08. Archived 2 Aprili 2008 at the Wayback Machine.
  5. Moss, Corey. "Dr. Dre's Final Album Will Be Hip-Hop Musical", MTV News, 2002-04-03. Retrieved on 2007-08-09. 
  6. Ro 2007, p. 9
  7. Ro 2007, p. 10
  8. Kenyatta 2000, p. 14
  9. Ro 2007, p. 2
  10. Ro 2007, p. 11
  11. Past Winners Search – Dr. Dre. Grammy.com. Iliwekwa mnamo February 5, 2013.
  12. Past Winners Search – Andre Young. Grammy.com. Iliwekwa mnamo February 5, 2013.
  13. Grammy Awards History. Rock On The Net. Iliwekwa mnamo March 7, 2015.
  14. Documentary 'Unity' Set for Aug. 12 Release with 100 Star Narrators. Variety (April 22, 2015). Iliwekwa mnamo May 1, 2015.
  15. The Defiant Ones at the Internet Movie Database
  16. "DPG 4 Life" Movie Cast Released. hiphopdx.com.
  17. Harold House Moore plays to Dr. Dre in All Eyez on Me. www.lamanagement.co. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 2019-06-17.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]