Chris Brown
|
|
Unganisha! Imependekzwa makala hii iunganishwe na Chris Brown (mwimbaji). Ili kupata sababu angalia ukurasa wa majadiliano. |
| Chris Brown | |
|---|---|
Brown akitumbuiza huko mjini Seattle Jingle Bell Bash 8
|
|
| Maelezo ya awali | |
| Jina la kuzaliwa | Christopher Maurice Brown |
| Amezaliwa | 5 Mei 1989 |
| Asili yake | Tappahannock, Virginia, Marekani |
| Aina ya muziki | Pop, R&B, hip hop, dance |
| Kazi yake | Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, dancer, mwigizaji |
| Aina ya sauti | Tenor[1] |
| Miaka ya kazi | 2005–mpaka sasa |
| Studio | Jive, Zomba, LBW |
| Tovuti | www.chrisbrownworld.com |
Christopher Maurice "Chris" Brown (amezaliwa tar. 5 Mei 1989) ni msanii wa rekodi za muziki na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Ameanza kutoa rekodi yake ya kwanza mwishoni mwa 2005 yenye jina sawa na lake, yaani, Chris Brown akiwa na umri wa miaka 16. Albamu ina kibao kikali cha "Run It!", ambacho kilifikia nafasi ya juu kwenye Billboard Hot 100, na kumfanya Brown kuwa msanii wa kiume wa kwanza kushika nafasi ya kwanza tangu Montell Jordan kuwa naye kutoa kibao na kushika nafasi ya kwanza kwenye chati.[2] Albamu imeuza nakala zaidi ya milioni mbili kwa Marekani na kutunukiwa platinamu mbili mfululuzo na Recording Industry Association of America (RIAA).[3]
Albamu ya pili ya Brown, Exclusive ilitolewa duniani kote mnamo mwezi wa Novemba 2007. Ilitamba na vibao vyake vikali vilivyopata mafanikio makubwa kabisa; kibao chake cha pili kwa U.S. "Kiss Kiss" akimshirikisha T-Pain na "With You", ambao ulishika nafasi ya pili kwenye chati za Billboard Hot 100.[4][5] Brown ametoa toleo la hali ya juu la albamu lililokwenda kwa jina la The Forever Edition. Kibao cha kwanza kutoka kwenye albamu hiyo ni "Forever", kilitolewa mnamo mwezi wa Mei 2008 na kushika nafasi ya pili kwenye chati za Billboard Hot 100.[6] Exclusive has been certified Platinum by the RIAA.[3]
Licha ya kupata mafanikio makubwa akiwa kama msanii wa kujitegemea, Brown amepata kushirikishwa kwenye vibao vingine vikali kama vile "No Air", aliimba pamoja na Jordin Sparks, "Shortie like Mine" sambamba kabisa na rapa Bow Wow na "Shawty Get Loose" na Lil Mama na T-Pain. Kibao hicho kilishika nafasi ya tatu, namba tisa na kumi kwenye chati za Billboard Hot 100 mfululizo.[7][8][9] Kutokana na utaratibu wake wa kucheza, Brown amefananishwa kujulikana kama wasanii wa R&B kama vile Usher na Michael Jackson, wote hudokezwa kama wao ndiyo wenye athira nzima ya muziki wa Brown.[10] Mnamo 2009, Brown alishtakiwa kwa kosa la kumshambulia mwandani wake - mwimbaji Rihanna, na akapigwa kifungo cha nje cha miaka mitano na miezi sita ya mawasiliano ya kihuduma-kijamii na mpenziwe.
Yaliyomo |
1989–2004: Maisha ya awali na shughuli za mwanzo [hariri]
Diskografia [hariri]
- Chris Brown (2005)
- Exclusive (2007)
- Graffitii (2009)
- F.A.M.E. (2011)
- Fortune (2012)
Filmografia [hariri]
| Televisheni | |||
|---|---|---|---|
| Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
| 2006 | Christmas in Washington | Chris Brown | television special (Turner Network Television) |
| 2007 | The O.C. | Will Tutt | vipengele vitatu |
| 2008 | The Suite Life of Zack and Cody | Chris Brown | nyota mwalikwa |
| 2011 | Tosh.O | Chris Brown | mwalimu wa densi |
| Filamu | |||
| Mwka | Jina | Uhusika | Maelezo |
| 2007 | Stomp the Yard | Duron | small role/film debut |
| This Christmas | Michael 'Baby' Whitfield | uhusika mkuu | |
| 2009 | Blood Rogues | Christopher | |
| 2010 | Takers | Jessie Attica[11] | Executive Producer |
| 2012 | Think Like A Man | ||
Marejeo [hariri]
- ↑ Moody, Nekesa Mumbi (2007-11-06). Music Review: Chris Brown CD. Yahoo!. Rudishwa juu ya 2009-01-17.
- ↑ Chris Brown - Run It! Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
- ↑ 3.0 3.1 RIAA - Gold & Platinum. RIAA. Rudishwa juu ya 2009-01-12.
- ↑ Reuters (2007-11-02). R&B singer Chris Brown tops U.S. singles chart. Yahoo! 7 Music. Rudishwa juu ya 2008-08-14.
- ↑ Chris Brown - With You Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
- ↑ Chris Brown - Forever Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
- ↑ Billboard - Updated Album Charts from the most Trusted Music Magazine
- ↑ Shortie like Mine Chart Track. Accharts. Accessed 16 Agosti 2008.
- ↑ Lil Mama and Chris Brown - Shawty Get Loose - Music Charts. Accharts. Accessed 16 Agosti 2008.
- ↑ Billy Johnson, Jr. (2008-05-01). Usher, Has Chris Brown Taken Your Spot?. Yahoo! Music. Rudishwa juu ya 2008-08-16.
- ↑ Adler, Shawn (2008-10-02). Chris Brown Dances Around Bullets In Upcoming Film 'Bone Deep'. MTV. MTV Networks. Rudishwa juu ya 2009-02-10.
Viungo vya Nje [hariri]
|
|||||||||||||||||||||||||||||
| Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chris Brown kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |