Rose Ndauka
Rose Ndauka (amezaliwa 7 Oktoba 1989) ni mwigizaji wa filamu kutoka Tanzania. Rose ni mke wa Haffiyy Mkongwa na mama wa watoto wawili mmoja aitwaye Princess Naveen na mwengine ni Prince Haleem.
Alipata elimu yake katika shule ya sekondari Zanaki - Dar es Salaam ambapo alimaliza mwaka 2008.
Toka alipokuwa mdogo sana Rose alipenda kuigiza. Kipaji chake hicho kiligunduliwa na mama yake mzazi kabla ya yeye mwenyewe kuamua kujiingiza rasmi kwenye tasnia ya filamu nchini.
Rose alionekana kwa mara ya kwanza kwenye filamu ya “Swahiba” aliyoigiza kama “Aisha” mnamo mwaka 2007. Filamu hii ilipigiwa kura kama filamu bora ya mwaka na kituo cha redio cha Clouds FM.
Baada ya filamu hiyo Rose aliweza kupata nafasi ya kuigiza katika filamu mbalimbali zikiwemo Mahabuba na Solemba. Nyota yake ilionekana sana pale alipoigiza filamu ya Deception na marehemu Steven Kanumba kama mmoja wa waigizaji wakuu pamoja na Lost Adam aliyoigiza na mkali mwingine wa bongo movies Jacob Steven “JB”
Mwaka 2010 Rose Ndauka alifungua kampuni yake mwenyewe ya “Ndauka Entertainment”, pia alipata nafasi ya kuigiza kwenye filamu inayohusu mauaji ya halaiki ya Rwanda iliyopewa jina la “Rwanda baada ya vita” (ama Urwanda nyuma u'genocide kwa Kinyarwanda).
Rose ni director wa kampuni ya HRD radiator company[1] wanashughulika na services, designing na air conditioning.
Mwaka huohuo chini ya kampuni yake Rose alitoa filamu mbili za “Bad Girl” na “The Diary” ambazo zilifanya vizuri sana sokoni.
Mashabiki wake wanapenda kumuita “Rosie” na mara nyingi amekuwa akipata “attention” kubwa kwenye vyombo vya habari na magazeti kutokana na mvuto wake na umbo lake zuri.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.hrdradiator.co.tz