Peter Bwimbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Peter D. Bwimbo alikuwa mlinzi mkuu wa kwanza wa mwalimu Julius Nyerere katika kipindi cha kabla ya uhuru na baada ya uhuru na miongozi mwa watu wa mwanzo walioasisi taasisi ya usalama wa taifa Tanzania.

Kuzaliwa[hariri | hariri chanzo]

Peter Bwimbo alizaliwa tarehe 4 Machi 1929 katika kijiji cha Bulamba ndani ya kisiwa cha Wilaya ya Ukerewe, baba yake akijulikana kama Bwimbo bin Ekara na mama yake akiitwa Karyanja binti Mugheta.

Wakati Bwimbo anazaliwa ulikuwa ni msimu wa kupalilia magugu katika mashamba ya mazao ya chakula, hivyo alipewa jina la Mabagara huku akiendelea kupewa majina mengine mbalimbali likiwemo jina la Ekara ambalo ni jina la babu yake mzaa baba na jina lingine ambalo aliwahi kuipewa ni Magurira na kulingana na tamaduni za majina yao,inasemekana majina hayo yalikumkubali na kama yasingemkubali basi angekubana na tatizo la kusumbuliwa na mizimu [1]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Katika kipindi hicho cha ukuaji wa Peter Bwimbo, upatikanaji wa elimu ulikuwa mgumu sana lakini baba yake Peter ndiye aliyekuwa mtu wa mwanzo aliyeanza kumfundisha Peter kusoma katika chumba kidogo walichokuwa wakisoma nyakati za usiku huku wamewasha taa ya chemli, yeye pamoja na dada zake walianza kwa pamoja lakini baadae baba yao aliamua kuacha kufundisha watoto wengine kwa sababu walikuwa hawaelewi na aliendelea kumfundisha Peter peke yake.

Siku moja katika mwaka 1942 wakati Peter Bwimbo anauza miwa nje ya nyumba yao,alikuja kijana mmoja aitwae Masamaki Bin Kabisi na kuomba maji ya kunywa, kijana huyo alikuwa amevalia mavazi ya shule na Peter alipomuona alivutiwa na mavazi hayo na kumuuliza ni wapi anasoma na kijana yule alijibu kuwa anasoma native adminstration Bwiru Mwanza.

Baada ya Peter kuvutiwa na kusoma,alimuomba baba yake ampeleke shule na bahati nzuri baba yake alikubali na kuamua kumpeleka katika shule aliyoelekezwa na Masamaki. Alipofika shuleni alihojiwa kama aliwahi kusoma shule yoyote lakini alisema kuwa hajawahi kusoma, ndipo walimu walimfanyia usaili na kukubali aanze na darasa la kwanza, Peter alianza shule akiwa na umri wa miaka 14.

Mwaka 1949 alijiunga na chuo cha ualimu cha Pasiansi Mwanza na mwaka uliofuatia baada ya likizo ya kwanza Peter Bwimbo alianza rasmi mchakato wa kujiunga na jeshi la polisi na mnamo tarehe 2 Machi alipatiwa namba ya polisi A 518 na kuanza kulipwa mshahara wa shilingi sabini na tano.

Kwa wakati huo katika idara za jeshi walikuwa wanaajiriwa wanaume pekee yako lakini kufikia mwaka 1962 baada ya uhuru ndipo askari wakike walianza kujiunga na idara za polisi, Mwalimu Julius Nyerere aliomba serikali ya ilete maafisa wa kike ili kutoa mafunzo kwa askari wa wanawake, na serikali ya Uingereza ilikubali na kumleta Doreen Ann Prissick ambae alianza kufundisha askari wa kike kwa wakati huo Peter Bwimbo alikuwa yupo katika kikosi cha Special Branch.

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

Peter Bwimbo mbali na taaluma za kiaskari na usalama [2] alizipitia lakini pia ni muandishi, na kitabu alichokiandika kinaitwa Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere [3]kilichochapishwa na Mkuki na Nyota mwaka 2016.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Bwimbo, D. M. (2015). Peter DM Bwimbo. Oxford: Mkuki na Nyoka Publishers. ISBN 978-9987-753-50-5. OCLC 1102471977. 
  2. "Bodyguard reveals where Nyerere hid during mutiny". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-02-06. 
  3. D.M, Bwimbo, Peter (2015-11-03). Peter DM Bwimbo: Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere (kwa Kiswahili). Mkuki na Nyota Publishers. ISBN 978-9987-753-32-1. 
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Peter Bwimbo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.