Msalvia (mmea)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msalvia
Msalvia (Salvia divinorum)
Msalvia
(Salvia divinorum)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Lamiales (Mimea kama guguchawi)
Familia: Lamiaceae (Mimea iliyo mnasaba na mnanaa)
Jenasi: Salvia
L.
Spishi: S. divinorum
Epling & Játiva

Msalvia (ujulikanao pia kama sage of the diviners, ska maría pastora, seer's sage, yerba de la pastora ama kwa kifupi salvia; jina la kisayansi Salvia divinorum) ni mmea ambao utumizi wa majani yake kwa njia ya kutafuna, kuvuta kama sigara au kupika kama chai unasababisha namna ya ulevi.[1] Majani ya mmea huu yana vidonge aina ya opioindi zinazosababisha ukumbusho-wazimu (hallucination).[2] Kwa vile mmea huu haujifanyiwa utafiti kwa kina, madhara yake na usalama wa matumizi yake kwa muda mrefu bado haujathibitishwa.

Majani yake hutumika pia kusafisha meno.

Asili na historia[hariri | hariri chanzo]

Asili ya mmea huu ni nchi ya Mexico na humea kiasilia katika msitu wa Sierra Mazateca ya Oaxaca kwenye vivuli vilivyo na unyevu. Msalvia hufikia urefu wa kima zaidi ya mita moja na huwa na shina mraba lisilo na kitu ndani kama mimea mingine ya familia ya mnanaa Lamiaceae. Leo msalvia pia hukuzwa nyumbani na hupandwa vipandikizi vya tawi au shina lake kwa vile mmea huu hutoa mbegu kwa uchache na ugumu sana.

Sheria[hariri | hariri chanzo]

Mmea Msalvia umeruhusiwa katika nchi nyingi lakini matumizi yake hudhibitiwa nchini Australia, Ubelgiji, Brazil, Canada, Denmark, Estonia, Finland, Ujerumani, Italia, Japan, Korea Kusini, Poland, Hispania, Uswisi, Armenia na sehemu nyingine Marekani.[3][4] Hata Vile mmea wa msalvia umeenea sehemu tofautitofauti na miche yake huuzwa na wakulima wa miti no dawa katika nchi nyingine.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Salvia divinorum". Drugs.com. 2018. Iliwekwa mnamo 22 June 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Butelman, Eduardo R; Kreek, Mary Jeanne (2015). "Salvinorin A, a kappa-opioid receptor agonist hallucinogen: Pharmacology and potential template for novel pharmacotherapeutic agents in neuropsychiatric disorders". Frontiers in Pharmacology 6. doi:10.3389/fphar.2015.00190. 
  3. Siebert (Legal status).
  4. Erowid (Legal status).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]