Kima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kima
Kima buluu
Kima buluu
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Nusuoda: Haplorrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na kima)
Oda ya chini: Simiiformes (Wanyama kama kima)
Ngazi za chini

Catarrhini (Kima wa Dunia ya Kale)
Platyrrhini (Kima wa Dunia Mpya)

Dume mdogo White-fronted Capuchin (Cebus albifrons)

Kima ni mamalia yeyote wa hali ya juu katika makundi ya cercopithecoid (kima wa Dunia ya Kale) au "platyrrhine" (Kima wa Dunia Mpya). Mamalia wote wa kima cha juu wasio prosimians au sokwe ni nyani. Kuna takribani spishi 264 wanaofahamika wa kima wanaowakilisha kundikubwa la mamalia wa hali ya juu. Kima huonwa kama ni mwenye akili sana na tofauti na sokwe; kima daima huwa na mikia. Kima wa Dunia ya Kale wanafanana zaidi na sokwe kuliko kima wa Dunia Mpya.


Yaliyomo

[hariri] Asili

Kutokana na kamusi ya kiingereza ya Oxfoid neno la kimombo ‘monkey’ lenye maana ya kima lilitokana na simulizi za kijerumani ya Reynard the Fox ya mwaka 1580. Katika simulizi hiyo mhusika aliyeitwa Moneke alikuwa ni mtoto wa Martin aliyekuwa sokwe. Neno Moneke laweza kuwa linaweza kuwa linatokana na lugha ya Kitaliano ‘monna’ lenye maana ya sokwe jike. Neno Moneke limedumu sana kutokana na umaarufu wa ‘Reynard The Fox’.

[hariri] Tabia

Kima wanaukubwa tofauti kutoka milimita za urefu 140 – 160 (pamoja na mkia) na uzito wa gramu 120 mpaka 140, mpaka urefu wa mita moja wa kilo 35. Wachache huishi kwenye miti wakati wengine huishi kwenye savana. Chakula chao ni matunda, majani, mbegu, maua, mayai na wanyama wadogo (ikijumuishwa wadudu na buibui). Kima wote wa dunia mpya wana mikia tofauti na wa dunia ya kale. Baadhi ya kima wana uoni wa rangi na wengine hawana. Huku kima wa dunia mpya wakiwa na macho kwa mbele walionekana tofauti hata baina yao hasa pua, mashavu na sehemu ya nyuma kwa ujumla.

[hariri] Uanishaji

Common Squirrel Monkey
Crab-eating Macaque katika Thailand

Ifuatayo ni orodha ikionesha familia za kima.

ODA PRIMATES
Nusuoda Strepsirrhini: komba, koni na lemuri
Nusuoda Haplorrhini
Oda ya chini Tarsiiformes
Familia Tarsiidae: komba vidole-virefu
Oda ya chini Simiiformes: kima
Oda ndogo Platyrrhini: kima wa dunia mpya
Familia Cebidae
Familia Aotidae
Familia Pitheciidae
Familia Atelidae
Oda ndogo Catarrhini: kima wa dunia ya kale
Familia ya juu Cercopithecoidea
Familia Cercopithecidae: kima, ngedere, mbega, makaku na nyani
Familia ya juu Hominoidea
Familia Hylobatidae: masokwe wadogo
Familia Hominidae: masokwe wakubwa na binadamu

[hariri] Mahusiano na binadamu

Spishi tofauti za kima wanamahusiano na binadamu baadhi yao hufugwa kama wanyama wa nyumbani na hutumika kama kifani cha binadamu kwenye maabara na safari ya angani. Pia huwahudumia binadamu wenye udhaifu. Kuna baadhi ya maneno kama huonekana kama wanyama waharibifu wa mazao [1] Kima ambao pia wapo kwenye mbuga ya watalii lakini hugeuka kama kitishio kwa watalii huona kama kuna kikwazo kwa binadamu hivyo tatizo dogo. Kwenye dini huwakilisha warevu.

[hariri] Kama huduma kwa watu wasiojiweza

Baadhi ya mashirika yamekuwa wakiwafunza kima wa wakapuchini kama wasaidizi kuwasaidia watu wenye matatizo ya uti wa mgongo na matatizo mengine ya kutembea. Baada ya mafunzo kutosha kima hawa huweza kuwahudumia barabara walemavu wakiwa ndani ya nyumba, kima husaidia kupika kuosha uso na kufungua chupa za vinywaji.

[hariri] Kwenye tafiti

Covance kima wa maabara huko, Vienna, Virginia, 2004–05

Kima aina ya Macaques wale wa Afrika Green Monkeys, hutumika kwenye tafiti nyingi aidha kwa kukamatwa porini au kulazimiswa. Hutumika sana kutokana na uwezo wao mkubwa wa kubeba vitu, kuzaliana kwa muda mfupi na kufanana kwao sana kisaikolojia na kimaumbile na binadamu.

[hariri] Angani

Sam, aina ya rhesus macaque, alirushwa angani, umbali wa maili 55 (89 km) na NASA katika 1959.

Nchi nyingi zinawatumia kima kama sehemu yao ya tafiti za anga kujumuisha marekani na Ufaransa. Kima wa kwanza kwenda angani aliitwa Albert IIi, ambaye aliruka angani na roketi ya marekani, mnamo june 14,1949.

[hariri] Kama chakula

Ubongo wa kima unaliwa kama chakula kitamu huko Asia ya kusini, China na Afrika [2]. Kwa taratibu ya dini ya kiislamu kula nyani ni marufuku kabisa. Hata hivyo kima huliwa sehemu nyingine ya Afrika, ambako nyama yake huuzwa kama nyama ya msituni”

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine