Mkoa wa Équateur
Mkoa wa Ikweta Ekwatéli / Équateur |
|
Mahali pa Mkoa wa Équateur katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | |
Majiranukta: 00°04′N 18°16′E / 0.067°N 18.267°E | |
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
---|---|
Wilaya | 7 |
Mji mkuu | Mbandaka |
Serikali | |
- Gouverneur | |
Eneo | |
- Jumla | 103,902 km² |
Idadi ya wakazi (1998) | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,626,606 |
Mkoa wa Équateur (Mkoa wa Ikweta) ni mmoja ya mikoa 26 ya kujitawala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Idadi ya wakazi wake ni takriban 1,626,606. Mji mkuu ni Mbandaka.
Mkoa huu ulianzishwa kutokana na ugawaji mpya wa mikoa kadiri ya katiba ya Kongo ya mwaka 2005. Kabla yake ilikuwa sehemu ya jimbo la Equateur pamoja na mikoa ya sasa ya Ubangi-Kaskazini, Mongala, Ubangi-Kusini na Tshuapa. Kabla ya kuingizwa katika jimbo la Equateur wakati wa rais Mobutu Sese Seko uliwahi kuwa mkoa wa pekee kati ya 1962-1966 kwa jina la Cuvette-Centrale.
Eneo la mkoa huu liko katika kaskazini-magharibi ya Kongo kando ya mto Kongo. Upande wa magharibi unapakana na nchi ya Kongo-Brazzaville.
Sehemu kubwa ya Hifadhi ya Taifa ya Lomako Yokokala iko ndani ya mkoa huu. Hifadhi hii inajulikana hasa kwa sababu ndiko mahali pekee duniani wanapoishi nyani kubwa wa Bonobo wanaohesabiwa kati ya hominidi.
Picha
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
Équateur | Ituri | Kasai | Kasai Mashariki | Katanga Juu | Kinshasa | Kivu Kaskazini | Kivu Kusini | Kongo Kati | Kwango | Kwilu | Lomami | Lomami Juu | Lualaba | Lulua | Mai-Ndombe | Maniema | Mongala | Sankuru | Tanganyika | Tshopo | Tshuapa | Ubangi Kaskazini | Ubangi Kusini | Uele Chini | Wele Juu | |
+/- |
Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Équateur kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |