LearnToPlayMusic.com

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanafunzi akijifunza kupiga Gitaa

LearnToPlayMusic.com ni kampuni ya uchapishaji wa nakala na majarida kuhusu elimu ya muziki iliyoanzishwa mwaka wa 1979 (kama Koala Music Publications), huko Adelaide, Australia Kusini na wapiga gitaa Gary Turner (mwanamuziki) na Brenton White.

Kitabu cha kwanza kilichochapishwa na LearnToPlayMusic.com kilikuwa Progressive Rhythm Guitar, [1] kikifuatiwa na Progressive Lead Guitar na Progressive Guitar Method (Kitabu cha kwanza), [2] [3] na ndicho kilikuwa kitabu cha mwisho ambacho kimeuza zaidi ya nakala milioni sita. LearnToPlayMusic.com imechapisha zaidi ya mada 450 za kipekee, na toleo zake zimetafsiriwa katika lugha tisa. [4] Mnamo mwaka wa 1982, kampuni hii ilizidi kukuwa hadi katika masoko ya Marekani na kimataifa, yenye makao yake makuu huko Costa Mesa, California .

Bidhaa za kampuni hii zinahusisha mahitaji ya muziki katika aina nyingi tofauti tofauti za muziki, zikiwemo; Blues, Rock, Classical, Country, Jazz, Heavy Metal, Folk, Gospel, Soul, Hip hop, Funk, Reggae, na R&B . Ala zinazofundishwa ni pamoja na Gitaa, Piano, Saksafoni, Ukulele, Flute, Rekoda, Banjo, gitaa la Bass, Mandolin, Ngoma, Kinanda ya Kielektroniki, Kuimba, Baragumu, Harmonica, Clarinet, Violin, na Filimbi ya Tin. [5]

Ubunifu wa LearnToPlayMusic.com unakuja kuonekana pale kampuni hii inakuwa ndio wachapishaji wa kwanza wa elimu ya muziki kupitia kanda za kaseti, CD na DVD kwenye bidhaa zao za vitabu. Mnamo mwaka 1999, kampuni ilibadilisha chapa kutoka Koala Music Publications hadi LearnToPlayMusic.com kama sehemu ya mkakati wa kuunda Midia Mpya na mbinu na programu za uwasilishaji kwa njia ya kidijitali. Bidhaa za kampuni hiyo zinasambazwa na Kundi la Mauzo ya Muziki huko Ulaya, Soko la Muziki nchini Uingereza, Shirika la Hal Leonard nchini Australia, na Charles Dumont & Sons nchini Marekani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Progressive rhythm guitar / [by] Gary Turner & Brenton White". National Library of Australia. Iliwekwa mnamo 9 May 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Progressive lead guitar / by Gary Turner and Brenton White". National Library of Australia. Iliwekwa mnamo 9 May 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Progressive guitar method / by Gary Turner & Brenton White". National Library of Australia. Iliwekwa mnamo 9 May 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. "Pro Music Catalogue". Pro Music Australia. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-31. Iliwekwa mnamo 9 May 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "LearnToPlayMusic.com Official Website". LearnToPlayMusic.com. Iliwekwa mnamo 9 May 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)