Gitaa
Gitaa ni ala ya muziki yenye nyuzi 4 hadi 12 zinazokazwa na kupigwa kwa kudonia nyuzi kwa kidole au kucha.
Gitaa huwa na bodi yake ambayo ni sanduku la ubao na juu yake shingo ambako nyuzi zinafungwa na kukazwa . Gitaa ya kawaida huwa na nyuzi 6. Bodi ya kawaida ina uwazi ndani yake inayopazia sauti ya nyuzi. Vidole vya mkono mmoja vinakaza nyuzi sehemu za shingoni na kutawala sauti ya uzi kuwa juu au chini. Vidole vya mkoni mwingine vinapiga nyuzi juu ya bodi na kuleta mipapatiko inayotoa sauti.
Kuna pia gitaa za umeme ambako kifaa kinachukua mipapatiko ya uzi na kuibadilisha katika umeme wa aina tofauti inayosikika kwenye kipazia sauti. Aina hii haihitaji bido yenye uwazi ndani yake.
Gitaa hutumiwa kwa muziki ya klasiki na pia kwa muziki ya rock.
Viungo vya Nje [hariri]
- Stalking the Oldest Six-String Guitar
- Guitar physics
- International Guitar Research Archive
- The first rock guitars
- Online Guitar Tuner - Standard Tuning.
- Modern Guitarist - News, reviews and articles.