Nyuzi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyuzi ni kizio cha kupimia pembe . Msingi wake ni mzunguko kamili wa duara unaogawiwa kwa sehemu 360. Kwa kawaida nyuzi moja huandikwa kama 1°.
Nusuduara ina 180°. Pembemraba ina 90°. Jumla ya pembe ndani ya pembetatu ni 180°, ndani ya mstatili ni 360°.
Historia[hariri]
Asili ya hesabu hii huaminiwa kuwa katika Babeli ya Kale. Wababeli walihesabu mwaka kuwa na siku 360 na wakitazama nyota waliona ya kwamba kila siku zilihama takriban kiwango cha 1/360 cha duara.
Katika jiometria muundo huu ulielezwa kimsingi na mwanaastronomia Hipparchos wa Nikaia (190 KK–120 KK).