Kungwi ni ndege mbua wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Striginae katika familia Strigidae. Spishi nyingine zinaitwa kokoko. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi. Wana mgongo kwa rangi ya kahawa au kijivu mwenye madoa meupe, na mbele yao ni nyeupe yenye madoa au michirizi nyeusi au kahawia. Spishi nyingi zina vishungi viwili vya manyoya vinavyofanana na masikio. Kungwi hula mamalia wadogo na wakubwa kiasi hasa (mpaka paa mdogo) lakini ndege, watambaazi na wadudu pia. Kokoko-walasamaki hula samaki hasa. Huwinda usiku. Kwa kawaida jike huyataga mayai 2 lakini 1-5 inawezekana. Tago lao ni chini, mitini, kwenye miamba iliyojitokeza nje na hata kwenye vishubaka vya madirisha.
Spishi za Afrika [hariri]
- Bubo africanus, Kungwi Madoa (Spotted Eagle Owl)
- Bubo ascalaphus, Kungwi-jangwa Pharaoh Eagle Owl)
- Bubo bubo, Kungwi wa Ulaya Eurasian Eagle Owl)
- Bubo capensis, Kungwi Kusi (Cape Eagle Owl)
- Bubo cinerascens, Kungwi Kijivu (Greyish Eagle Owl)
- Bubo lacteus, Kokoko (Verreaux's Eagle Owl)
- Bubo leucostictus, Kungwi wa Akun (Akun Eagle Owl}
- Bubo poensis, Kungwi wa Fraser (Fraser's Eagle Owl)
- Bubo shelleyi, Kungwi wa Shelley (Shelley's Eagle Owl)
- Bubo vosseleri, Kokoko wa Usambara (Usambara Eagle Owl)
- Jubula lettii, Kungwi Manyoya-marefu (Maned Owl)
- Scotopelia bouvieri au Bubo bouvieri, Kokoko-mlasamaki Michirizi (Vermiculated Fishing Owl)
- Scotopelia peli au Bubo peli, Kokoko-mlasamaki Madoa (Pel's Fishing Owl)
- Scotopelia ussheri au Bubo ussheri, Kokoko-mlasamaki Mwekundu (Rufous Fishing Owl)
Spishi za mabara mengine [hariri]
Spishi za kabla ya historia [hariri]
- Bubo binagadensis (Mwisho wa Pleistocene ya Binagady, Azerbaijan)
- Bubo florianae (Mwisho wa Miocene}
- Bubo leakeyae (Mwanzo wa Pleistocene ya Tanzania)
- Bubo osvaldoi Cuban Horned Owl, (Mwisho wa Pleistocene ya Kuba)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pliocene ya Senèze, Ufaransa)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pliocene ya Rębielice Królewskie, Poland)
- Bubo sp. (Mwisho wa Pleistocene ya San Josecito Cavern, Mexiko)
- Pulsatrix arredondoi (Mwisho wa Pleistocene ya Cueva de Paredones, Kuba)