Kokoko-mlasamaki
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Kokoko-mlasamaki | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Kokoko-walasamaki ni ndege mbua wa jenasi Ketupa na Scotopelia katika familia Strigidae. Siku hizi wataalamu wengi wanawaainisha katika jenasi Bubo. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na wana mnasaba na kungwi. Wana mgongo kwa rangi ya kahawa au kijivu mwenye madoa meupe, na mbele yao ni nyeupe yenye madoa au michirizi nyeusi au kahawia. Spishi za Ketupa zina vishungi viwili vya manyoya vinavyofanana na masikio. Ndege hawa wanatokea karibu na mito na maziwa katika miitu minene. Huwinda usiku na hula samaki hasa lakini amfibia na wanyama wadogo pia. Jike huyataga mayai 1 au 2 lakini mara nyingi kinda moja aishi tu. Kwa kawaida tago lao ni kwenye mti mkubwa mara nyingine katika shimo la mwamba.
Spishi za Afrika [hariri]
- Scotopelia bouvieri au Bubo bouvieri, Kokoko-mlasamaki Michirizi Vermiculated Fishing-owl)
- Scotopelia peli au Bubo peli, Kokoko-mlasamaki Madoa (Pel's Fishing-owl)
- Scotopelia ussheri au Bubo ussheri, Kokoko-mlasamaki Mwekundu (Rufous Fishing-owl)
Spishi za mabara mengine [hariri]
- Ketupa blakistoni au Bubo blakistoni (Blakiston's Fish )wl)
- Ketupa flavipes au Bubo flavipes {Tawny Fish Owl)
- Ketupa ketupu au Bubo ketupu {Buffy Fish Owl)
- Ketupa zeylonensis au Bubo zeylonensis (Brown Fish Owl)