Joseph Fourier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joseph Fourier
Kwenye kaburi la Fourier mjini Paris

Jean Baptiste Joseph Fourier (21 Machi 1768 - 16 Mei 1830) alikuwa mtaalamu wa hisabati na fizikia kutoka nchini Ufaransa.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alionekana kuwa na vipaji vikubwa alipokuwa mwanafunzi shuleni huko Auxerre.

Alipofikia umri wa miaka 18 alipewa kazi ya profesa palepale.

Mwaka 1705 alihamia Paris akawa profesa wa hisabati.

Pamoja na Napoleon Bonaparte alikwenda Misri mwaka 1799 akashiriki katika utafiti wa nchi. Baada ya kurdi alikuwa mkuu wa mkoa wa Isère, baadaye wa mkoa wa Rhone.

Tangu mwaka 1815 aliishi mjini Paris akawa Katibu wa akademia ya sayansi.

Pamoja na shughuli hizi zote, alifanya tafiti mbalimbali za kifizikia. Alieleza jinsi gani joto linapanua ndani ya gimba mango na hii huitwa Kanuni ya Fourier.

Alibuni pia mbinu kadhaa za hisabati zilizo muhimu kwa fizikia ya kisasa.