Mango
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mango ni moja kati ya hali maada. Maana yake ni imara, tofauti na kiowevu (majimaji) au gesi (kama hewa).
Katika hali mango atomi zinakaa mahali pamoja katika gimba hazichezi wala kutembea ndani yake. Kila atomi ina mahali pake. Gimba mango lina umbo, mjao na uzani maalumu. Umbo mango lina urefu, upana na kimo chake, tofauti na kiowevu kinachobadilisha umbo kufuatana na chombo chake au gesi isiyo na umbo wala mjao maalumu.
Kama mango inabadilika kuwa kiowevu tunasema inayeyuka. Kama inabadilika kuwa gesi au mvuke moja kwa moja tunaliita badiliko hili mvukemango.

