Mjao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Mjao inaeleza ukubwa wa gimba la hisabati (mchemraba, tufe, mcheduara) kwa kupima nafasi ya yaliyomo yake. Hupimwa katika vizio vya ujazo kama mita ujazo (m³) au sentimita ujazo (cm³). Kila gimba lenye urefu, upana na kimo huwa na mjao.

Alama yake ni V.

Hali halisi nje ya hisabati kuna njia mbili za kuangalia mjao wa gimba:

  • ujazo wa nje kwa jumla (kwa mfano kama kitu kinazamwa katika kiowevu kinasukuma kiasi gani cha kiowevu hiki?)
  • ujazo wa ndani (kwa mfano yaliyomo ya boksi au tangi)


Mifano ya kukadiria mjao wa magimba kadhaa[hariri | hariri chanzo]

Kadirio ya mjao ni Urefu x Upana x Kimo.

mchemraba mwenye urefu wa ukingo "a":
V = a\cdot a\cdot a = a^3
mchemstatili mwenye urefu wa kingo "a", "b" na "c":
V = a\cdot b\cdot c
tufe lenye rediasi "r"::
V = {{4}\over{3}} \pi \cdot r^3
mcheduara au mche mwenye eneo la kitako "A" na kimo "h":
V = A\cdot h