Frances Cabrini
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mama Frances Xavier Cabrini (15 Julai, 1850 – 22 Desemba, 1917) alikuwa mwanzilishi wa shirika la Masista Wamisionari wa Moyo Mtakatifu (kwa Kiingereza Missionary Sisters of the Sacred Heart).
Jumuiya hiyo ilianza Italia na kufanya kazi hasa Marekani kati ya wahamiaji kwa kujenga shule, hospitali na nyumba kwa watoto yatima.
Mwaka 1946 Mama Cabrini alitangazwa kuwa mtakatifu akiwa Mmarekani wa kwanza kutangazwa hivyo.
Sikukuu yake ni tarehe 22 Desemba.
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Frances Cabrini kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |