Emmanuel Adebayor
Emmanuel Adebayor | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Jina kamili | Sheyi Emmanuel Adebayor | |
Tarehe ya kuzaliwa | 26 Februari 1984 | |
Mahala pa kuzaliwa | Lome, Togo | |
Urefu | mita 1.95 | |
Nafasi anayochezea | Mshambuliaji | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | Manchester City | |
Namba | 25 | |
Klabu za vijana | ||
FC Metz | ||
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
2006- | Manchester City | |
Timu ya taifa | ||
2000 | Togo | |
* Magoli alioshinda |
Sheyi Emmanuel Adebayor (amezaliwa tar. 9 Februari 1985 mjini Lome, Togo) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Togo - mwenye asili ya Nigeria. Kwa sasa anaichezea klabu mashuhuri barani Ulaya ya Manchester City. Na pia huichezea Timu ya Taifa ya Togo.
Maswala ya Mpira
[hariri | hariri chanzo]Kuanza kwake kucheza mpira barani Ulaya
[hariri | hariri chanzo]Adebayor alihamia barani Ulaya akiwa na umri mdogo kabisa baada yakuacha klabu yake ndogo huko nchini Togo aliishi baadhi ya muda mrefu kidogo huko Ufaransa bila kuwa na timu lakini alikutwa akipenda mpira wa miguu tangu angali mdogo basi akawa anashiriki katika baadhi ya mechi za vijana katika mitaa ya Ufaransa, baadhi ya watu kutoka kwenye klabu ya Metz wakamuona nakumkubali kutokana na ufundi wa uchezaji wake wakawa wamemchukua nakumuweka kwenye Metz ya vijana lakini ya umri wa myaka 15 nakupandishwa kwenye Metz ya vijana wa miaka 17 na alicheza kama miaka miwili, baadae kutokana na uchezaji wake uzuri kocha wa timu ya kwanza ya Metz (timu kubwa) akaomba wampandishe kwenye timu kubwa nakushiriki na timu hiyo katika ligi ya kwanza ya Ufaransa (Ligue 1). Katika msimu wake wa kwanza, alicheza mechi tisa na alifunga mabao mawili tu. Katika msimu 2002-2003,Adebayor alifunga magoli 17 katika mechi 35.
Kuelekea AS Monaco
[hariri | hariri chanzo]Baada yakumuona kua ni mchezaji mzuri nakufunga magoli mengi katika msimu huo, klabu nyingi za Ufaransa zilipendelea kumnunua lakini klabu ya AS Monaco ilitoa pesa nzuri na ndio ilimchukua mchezaji huo katika mwaka wa 2003, na katika huo msimu alifunga magoli 7 katika mechi 17 alizozicheza katika ligi hiyo, Adebayor aliisaidia klabu hiyo ya Monaco kufika fainali katika Ligi ya klabu bingwa barani Ulaya (Champions League) kwakufunga magoli ma wili katika mechi kumi alizozicheza lakini klabu hiyo haikuchukua kombe ilifungwa magoli 2-1 na klabu ya Ureno iitwayo FC Porto
Kutoka AS Monaco nakuelekea FC Arsenal
[hariri | hariri chanzo]Tar 13 Januari 2006, Adebayor aliweka mkataba na klabu mashuhuri duniani na barani Ulaya kwa kiwango cha pesa milioni tatu paund (£3m, zilizokadiriwa) Adebaryor alipewa lakabu (Jina) la Baby Kanu (kanu mtoto) kutokana na namna alivyo kimaumbile nakumfanana kanu kwa kila kitu hadi uchezaji pia na Adebayor mchezaji anaependa tangu angali mdogo ni Kanu mchezaji mashuhuri barani Afrika na Ulaya na ulimwengu. Mechi yake ya kwanza katika Ligi kuu ya Uingereza Katika tar 4 Fubruari 2006,Adebayor alicheza mechi yake ya kwanza katika Ligi kuu ya Uingereza ilikua dhidi ya klabu ya Birmingham City na alifunga goli katika dakika ya 21 Katika mwaka 2005-2006 Hakuweza kushiriki na timu yake mpya ya Arsenal katika Ligi ya klabu bingwa barani Ulaya kwani alishiriki baadhi ya mechi na klabu ya Monaco na sheria ya chama cha mpira cha ulaya hakiruhusu kushiriki na timu mbili katika mashindano hayo kwa hiyo hakufaanikisha kucheza hata fainali dhidi ya timu Barcelona klabu kutoka Uhispania ni mashuhuri duniani pia, lakini alicheza na timu hiyo pindi mashindano hayo yalipokwisha mwaka ufwatao. Mechi maarufu aliyofunga goli la ufundi wa hali ya juu ilikua katika msimu wa 2006-2007 dhidi ya timu mashuhuri nyingine duniani iitwayo Manchester United ambayo alifunga goli la ushindi katika dakika za mwanzo na mechi hiyo ilichezeka katika uwanja wa Manchester uitwao Old Trafford
Adebayor mwaka 2008
[hariri | hariri chanzo]Tunaanzia Ijumatatu tar.4 machi dhidi ya AC Milan klabu kutoka Italia mashuhuri duniani pia katika mechi hiyo ilikua ya marejeo na Adebayor hakuwai funga goli la aina yoyote na timu yake hiyo ya Arsenal katika mashindano hayo lakini mechi ya marejeo dhidi ya AC Milan alifunga goli katika mechi hiyo iliyoisha 2-0 katika uwanja unaopatikana milano uitwao San Siro. Tar 13 Aprili katika ligi kuu ya Uingereza mechi nzuri ilikua dhidi ya Manchester United mechi hiyo iliisha 2-1 Adebayor alifunga goli moja katika mechi hiyo katika Uwanja wa Old Trafford. Lakini mwaka huo Arsenal haikuchukua kombe la aina yoyote katika msimu huyo, Adebayor alichaguliwa katika timu ya Ligi kuu ya Uingereza na pia goli la pili alilolifunga dhidi ya ya klabu maarufu Uingereza ya Tottenham Hotspur mechi hiyo iliitwa mechi ya siku ilikua nzuri sana, na goli alilolifunga liliitwa goli la msimu wa 2007-2008 katika ligi hiyo.Mwaka huo 2008 katika msimu wa kuhama hama kutokana na uchezaji wake mzuri ulionekana, klabu kubwa barani ulaya zilipendelea kumnunua kwakutoa pesa nyingi, Ilizungumzwa klabu kama Barcelona na AC Milan zilitoa pesa kiwango cha milioni thalathini ili kumnunua,lakini klabu yake ilikataa kumuacha mchezaji wake na mchezaji huo alikubali kubaki baada ya klabu hiyo kumzidishia mshahara na aliweka mkataba wakupokea paundi 80.000 za Kiingereza kwa wiki moja (£80,000),katika mwaka huu bwana Adebayor alifunga magoli matatu katika mechi moja na ilikua dhidi ya klabu Blackburn Rovers ya huko Uingereza mechi hiyo iliisha 4-0.
Timu yake ya taifa kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Adebayor namna ijulikanavyo ni mwenye asili ya Nigeria angalau amezaliwa Togo,yeye amechagua kuchezea timu ya taifa ya Togo kuliko kuichezea timu ya Nigeria. Yeye aliisaidia timu yake ya taifa ya Togo kwenda kombe la dunia la 2006 Ujerumani na kombe la Mataifa ya Afrika 2006 Misri , na katika kugombea tiketi ya kwenda kwenye kombe hizo mbili alifunga magoli 11,
Kombe la mataifa ya Afrika 2006 Misri
[hariri | hariri chanzo]alikua na matatizo na kocha wa Togo na alafu kocha katika mechi za mwanzo alimuweka benci kama vile kumuadabisha mpaka ikasemwa kua kuna uwezekano akaacha shindano hilo nakurejea nyumbani,lakini baadae aliendelea mazowezi na wenzake na timu yake ilitoka katika mashindano baada yakufungwa mechi zote, Adebayor alifukuzwa na chama cha mpira wa miguu huko Togo kutokana na matatizo ya malipo ya pesa waliyokubaliwa na chama hicho na yeye alikua katika watu waliopinga nakufanya fujo.
Kombe la dunia 2006 Ujerumani
[hariri | hariri chanzo]Adebayor aliisaidia timu yake ya taifa kuchukua tiketi yakwenda kombe la dunia lililofanyika Ujerumani mwaka 2006, Togo haikuonekana na ukali ambao ilionekana nao wakati wakuwania tiketi ya kwenda huko maana ilionekana timu isiocheza mpira mzuri na walitoka mapema katika shindano hilo na Adebayo mwenyewe katika shindani hilo hakufunga hata goli limoja.
Mchezaji bora Afrika 2009
[hariri | hariri chanzo]Tar. 10 mwezi wa Februari 2009, Bwana Adebayor alichaguliwa mchezaji bora barani Afrika baada ya kuwashinda wa chezaji Aboutreka kutoka Misri na Michael Essie mchezaji kutoka Ghana, na mwaka 2007 alichukua mchezaji bora barani Afrika kutoka BBC zawadi hiyo pia hugawiwa kila mwaka.
Zawadi na Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Monaco
[hariri | hariri chanzo]- Ligi ya klabu bingwa barani Ulaya (Champions League) na fasi ya pili: 2004
Arsenal
[hariri | hariri chanzo]Ushindi
- Kombe la Emirates: 2007
- Shindano la Amsterdam: 2007 na 2008
- Kombe la Carling Cup(Uingereza): 2006
Zawadi binafsi
[hariri | hariri chanzo]- goli la mwezi: Septemba 2007
- goli la msimu: 2007-2008
- mchezaji katika timu ya ligi kuu Uingereza (PFA Team of the Year): 2007-2008
- BBC mchezaji bora barani Afrika wa mwaka': 2007
- Mchezaji bora barani Afrika wa mwaka: 2008
- Mchezaji bora wa mwaka Togo: 2005, 2006, 2007, 2008
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Blogi ya Adebayor Ilihifadhiwa 21 Juni 2014 kwenye Wayback Machine.
- Kuhusu Emmanue Adebayor katika tovuti rasmi ya Arsenal Ilihifadhiwa 20 Aprili 2014 kwenye Wayback Machine.
- Adebayor katika Tovuti ya Chama cha mpira cha Ulaya
- Adebayor katika www.footballdatabase.com
- Emmanuel Adebayor career stats kwenye Soccerbase
- Kuhusu Adebayor katika Ligi kuu ya Uingereza Ilihifadhiwa 26 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
- Mchezaji bora barani Afrika mwaka 2007 katika BBC