Bamba la Cocos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bamba la Cocos.

Bamba la Cocos ni bamba la gandunia katika Pasifiki ya mashariki lililopo mbele ya pwani ya Amerika ya Kati. Jina lake limetokana na Kisiwa cha Cocos .

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ni bamba dogo lililopo chini ya bahari mbele ya pwani za Mexico, Guatemala, El Salvador, Nikaragua na Kosta Rika.

Linapakana na Bamba la Pasifiki, Bamba la Amerika ya Kaskazini, Bamba la Karibi na Bamba la Nazca. Upande wa kaskazini bamba dogo la Rivera lilijitenga na hilo la Cocos.

Upande wa magharibi na kusini bamba hilo linaachana na mabamba ya Pasifiki na ya Nazca na hapa kuna nyufa ambako magma hupanda juu ya kujenga migongo ya bahari. Upande wa mashariki bamba hilo linasukumwa chini ya Bamba la Karibi linalobeba nchi za Amerika ya Kati na kwenye kaskazini chini ya bamba la Amerika Kaskazini.

Tokeo lake ni safu za volkeno katika Amerika ya Kati, pamoja na volkeno Santa Ana yenye kimo cha mita 2,381 huko El Salvador. Tokeo jingine ni ukanda wa matetemeko ya ardhi yanayotokea mara kwa mara na kuelekea hadi Mexiko. Matetemeko makali ya Jiji la Mexiko (1995), ya El Salvador (2001) na ya Chiapas (2017) yalitokana na kuzama kwa bamba la Cocos chini ya mabamba ya Amerika Kusini na Karibi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]