Bamba la Pasifiki
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bamba la Pasifiki ni kati ya mabamba makubwa ya gandunia ya dunia yetu. Lipo chini ya bahari ya Pasifiki ikiwa ni bamba la gandunia kubwa kabisa. Maada yake ni miamba nzito ya gumawesi.
Mipaka [hariri]
Bamba la Pasifiki hupakana na mabamba ya Amerika ya Kaskazini, Juan Fuca, Cocos, Nazca, Antaktika, Australia na Ufilipino.
Mwendo na pete la moto [hariri]
Bamba lote lina mwendo wa kuelekea kaskazini-magharibi kwa mkasi wa sentimita 10 kwa mwaka.
Mwendo huu unaacha nafasi upande wa mashariki inayoonekana kama bonde la ufa kwenye msingi wa bahari. Upande wa magharibi bamba lajisukuma chini ya bamba la Ufilipino na tokeo lake ni mfereji wa Mariana.
Kando la bamba kuna volkeno nyingi zinazoitwa "pete ya moto".