Antonio Maria Gianelli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake.

Antonio Maria Gianelli (Cereta, karibu na Mantova, 12 Aprili 1789Piacenza, 7 Juni 1846) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika Jimbo Katoliki la Bobbio, Italia Kaskazini, kuanzia mwaka 1837 hadi kifo chake[1].

Katika juhudi zake kwa mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya watu, alianzisha mashirika ya kitawa ya Mabinti wa Bibi Yetu wa Bustani na Wamisionari wa Mt. Alfonsi.

Aliacha mfano mwangavu wa mtu aliyewajibika kusaidia maskini, kuokoa roho na kuinua maadili ya mapadri wake.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 19 Aprili 1925, halafu mtakatifu na Papa Pius XII tarehe 21 Oktoba 1951[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Sant'Antonio Maria Gianelli". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 17 September 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Saint Anthony Mary Gianelli". Saints SQPN. 7 June 2009. Iliwekwa mnamo 15 April 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.