Nenda kwa yaliyomo

Zubeda Hassan Sakuru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Zubeda Hassan Sakuru ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CHADEMA. Alichaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake kwa miaka 20152020. Vilevile alipata nafasi ya kuwa Naibu Waziri kivuli wa Maendeleo ya Jamii, Afya, Wanawake na Watoto. Mwaka 2019 aliteuliwa kuwa Waziri Kivuli wa Maji na Umwagiliaji.

Zubeda ana shahada ya Utawala katika Masuala ya Utumishi wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Shahada ya Uzamili ya Menejimenti ya Rasilimali Watu katika chuo hicho kilichopo Tanzania. Pia ana shahada ya Uzamili katika Sera Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza.

Ameendelea kufanya tafiti za sera za umma na ushauri wa uongozi. [1]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017