Ziwa Great Slave
| |
Nchi zinazopakana | Kanada, jimbo la Northwest_Territories |
Eneo la maji | km2 27,200 |
Kina cha chini | m 614 |
Mito inayoingia | Mito ya Hay, Slave, Taltson, Lockhart, Yellowknife |
Mito inayotoka | Mto Mackenzie |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
m 156 |
Ziwa Great Slave (kwa Kifaransa: Grand lac des Esclaves; kwa Kiingereza: Great Slave Lake) ni ziwa la pili kwa ukubwa katika maeneo ya Northwest Territories ya Kanada. Ni ziwa lenye kina kirefu zaidi katika Amerika Kaskazini likifikia mita 614 [1] na ziwa kubwa la tisa duniani. Urefu wake ni km 480 likiwa na upana wa km 19 hadi 109, hivyo kuwa na eneo la km2 27,200.
Jina linatokana na neno la utani la Maindio wa Cree kwa maadui wao waliokalia sehemu ya ziwa. Waliwaita "watumwa" na jina hili lilitafsiriwa na Wafaransa wa kwanza waliofanya biashara na Wacree na kuingizwa katika ramani zao wakiandika "Lac des Esclaves" (ziwa la Watumwa, walishika pia "mto wa watumwa"). Umbo hili la Kifaransa lilitafsiriwa baadaye kwa Kiingereza "Slave Lake", ilhali kuna "Great Slave Lake" na "Lesser Slave Lake", pia "Slave River".
Miji kwenye ziwa ni pamoja na: Yellowknife, Hay River, Behchoko, Fort Resolution, Lutselk'e, Hay River Reserve, Dettah na N'Dilo.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Wakati wa baridi kuna barabara ya magari kwenye barafu ya ziwa Great Slave
-
Hori ya kaskazini kwenye Ziwa Great Slave
-
Mto Hay ni kati ya mito inayochangia ziwa
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hebert, Paul (2007). "Encyclopedia of Earth". Washington, DC: Environmental Information Coalition, National Council for Science and the Environment. Iliwekwa mnamo 2007-12-07.
{{cite journal}}
: Cite journal requires|journal=
(help)
Tovuti za Nje
[hariri | hariri chanzo]- Picha za Lake Slave Lake Ilihifadhiwa 18 Julai 2012 kwenye Wayback Machine. kutoka Picsearch.com
Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ziwa Great Slave kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |